Naomba kujuzwa taratibu za kusafiri na silaha nje ya nchi

Joined
Apr 9, 2020
Posts
18
Reaction score
21
Habari za leo wakuu,

Naomba kujua je! unaruhusiwa kusafiri nje ya nchi ukiwa na bastola yako na ambayo unaimiliki kihalali? Kama jibu ni ndiyo ni taratibu zipi napaswa kuzifuata ili kukamilisha hilo mbali na taratibu zingine za migration?

Nawasilisha
 
Labda haujaeleweka.

Mfano wewe ni raia wa kawaida tu. Unakaa Tanzania. Unataka kwenda Kenya na Siraha yako. Haiwezekani. Unatakiwa uiache Tanzania. Ukifika Kenya ufanye taratibu za kibali cha kumiliki silaha nchini Kenya ndio ufanye utaratibu wa kuisafirisha ile silaha na documents zake ifike Kenya.

Mfano wa pili. Wewe ni raia wa Tanzania lakini shughuli zako unazifanyia Kenya. Itakupaswa uwe na vibali vya nchi zote kumiliki silaha.

Mfano wa tatu. Wewe Mtanzania unataka kwenda kazini kwako Kenya. Na una vibali vya kumiliki silaha vya nchi zote mbili. Ukifika kwenye ndege unaikabidhi ile silaha (mara nyingi zinakaa kwa captain kule kwenye ka ghetto kake) utapewa wakati wa kucheck out. Hauruhusiwi kukaa nayo kwenye cabin.
 
Mbona mifano yako yote umeizungumzia Kenya?? Europe je au America??
 

Asante sana kwa ufafanuzi mkubwa ulioutoa mkuu, nimeelewa mno.
 

Asante sana kwa ufafanuzi mkubwa ulioutoa mkuu, nimeelewa mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…