Sijajua kama unayaongea haya kwa uzoefu au ushabiki.
Ili useme juu ya utagaji wao inapaswa tuwe na mfano wa kulinganisha nao. Je unaposema hawana utagaji mzuri, utagaji wao ni mbaya kulinganisha na aina ipi?
Hao waliokwambia kuku anataga mayai 95 tu kwa mwaka, wanazungumzia mwaka wa utagaji au mwaka wa maisha ya kuku? Maana zitakuwa ni akili za ajabu kabisa kumhesabia kuku kataga mayai tisini kwa mwaka bila kuzingatia kuwa anaanza kutaga akifikisha miezi mitano.
Mimi acha nikupe uzoefu, maana Kuroiler ninawafuga. Hawa kuku kwa kuwalinganisha na kuku wa kienyeji wao wanataga zaidi, il ukiwalinganisha na kuku wa mayai hawafikii uwezo wao wa kutaga. Lakini kuna jambo la kujifunza kuwa, hawa kuku wa mayai wanapewa suppliments nyingi sana kufikia huo utagaji, kitu ambacho hatufanyi kwa Kuroiler na kienyeji.
Jambo la pili nikupe maarifa na uzoefu, Kuroiler wanataga kati ya mwezi wa nne na nusu kuelekea wa tano, jambo ambalo halitokei kwa kienyeji na kuku wa mayai. Layers hutaga miezi 6 na kienyeji ni mwezi wa 6 kuelekea 7 na pengine 8 kabisa kama chakula ni haba.
Kuhusu ukubwa wa mayai, kuroiler anataga mayai makubwa kuliko kuku wa mayai. Lakini labda swali la kujiuliza ikiwa unaamini vinginevyo au una experience tofauti ni JE, HAO KUKU ULIONAO NI KUROILER AU ALIYEKUUZIA NDIO KAKWAMBIA NI KUROILER?
Shida moja ni kuwa, Kuroiler wana rangi sawa tu na kuku wa kienyeji, hivyo kuwatambua uhalisia wao si rahisi kwa hiyo watu wengi huuuziwa kuku wasiowajua na huishia kupata famba.