Naomba kujuzwa utagaji wa kuku aina ya Kuroiler na SASSO

Naomba kujuzwa utagaji wa kuku aina ya Kuroiler na SASSO

natafuta hee breed
FB_IMG_1634801343555.jpg
FB_IMG_1634801348154.jpg
 
kroiler ni watagaji wazuri sana, changamoto ni soko la mayai. Ukiuza mayai ya kroiler kwa bei kama ya mayai ya layers huwezi pata faida na wateja wengi uswazi watapendelea mayai cheap ya layers. Lakini kama una wateja wako wa mayai ya chotara watako weza kununua kwa sh 12,000 hadi 15,000 kwa trei fuga mwanagu utapata faida.
 
Kweli kabisa hata mimi nafuga kroiler wanaangusha mayai ni balaa
Kuku aina ya saso/sasu wanakuwa na maumbo makubwa utagaji wa mayai kwao ni hafifu sana wana uzito na hivyo wanafaa kwa biashara ya nyama unaweza uza Sasu mmoja hadi kwa 40,000tsh na mtu akakubali tu maana wana uzito mkubwa.
Unawalisha chakula Cha kampuni gani na vip? Unachnganya na pumba au unawapa peke Cha dukani
 
Hahahaa huu uzi umenikumbusha 2016-2017 nilikuwa nafuga kuku aina ya sasso ndio walikuwa wameingia! hawa kuku sijawahi kuona nilifuga kuku 250 nami nililenga kupata mayai lakini yupo jamaa aliitwa ADAM NYAMANGE mkurugenzi wa mtandao wa kijani kibichi alinitembelea baada ya kuona kwenye mitandao nafuga kuku wakubwa sana alivyofika kuku wangu walikuwa na miezi 5 na walianza kutaga na utagaji wake sio MZURI sana huwa wanaruka Siku lakini wana maumbo makubwa sana! akaniambia kwa mayai hutafanikiwa weka nguvu kwenye kuwahudumia uuze nyama!!
Nilianza kutafuta masoko kuku walikuwa wakubwa sanaa tetea kg 4 nilikuwa na majogoo 2 wenye kilo 5.5 na kwa ladha sijawahi kula kuku watamu kiasi hicho!! kwa ukubwa wa wale kuku nilipata tenda bodi ya mikopo mwenge! na walinunua kuku mmoja sh 35000 mpaka 40000 jogoo wale wawili aliwanunua mzungu mmoja ambaye aliagiziwa kwangu akajitambulisha kuwa anashughulika na kuku wa sasso na chakula cha SILVERLAND alinunua mmoja 60000 na walipelekwa sabasaba!! nisiongope mradi ule niliufurahia kilichonikera nilipotaka vifaranga awamu nyingine sikupata tena baadae nikaona hawapatikani saso f1 nikahamia kwenye kuroiler!

Kuroiler mayai wanataga vizuri sana ila ladha na ukubwa hawajafikia kwa sasso,, hivi nilipumzika kwa kuku naanza mwaka huu!! Sasa niko kwenye nguruwe na mbuzi wa kisasa wa nyama!!

Ufugaji ukizingatia mbegu bora, chakula cha kutosha, mabanda rafiki, chanjo kwa wakati , research ya masoko ,kufuga kwa muendelezo yaani ujibrand haswaa kila wakati wateja wako wasikose bidhaa ufugaji unalipa ila uhamue haswaaa.
Sawa.
 
Habari za majukumu wanajamvi
Hivi ukiwalisha sasso formula ya broiler kwa miez miwil ya mwanzo wanaweza kufika kg 2 ndani ya miez miwili
 
uzi mzuri, kuna elimu hapa
Ndio mkuu tunahitaji hiyo elimu ili tuweze kufuga ufugaji wa kuku wenye tija kama nchi zilizoendelea sio kufuga kimazoea mathalani ufugaji wa kuku wa kienyeji binafs nauona kama ni ngumu kutengeneza faida kubwa kwani uzalishaji huchukua muda mrefu sana japo sisemi ufugaji wa kuku wa kienyeji ni mbaya hapana huo ni mtazamo wangu tu
 
Asante saana, kweli kuku wa Sasso kwa mayai sio ila kwa nyama wako safi sana. Mimi changamoto ninayokutana nayo kwa kuku hao kwa upande wangu wanaugua saana flue, macho na kuna wakati wanakua walegevu miguuni. nimepambana nao sana ila sijapata utatuzi wa kudumu.
 
Back
Top Bottom