Naomba kujuzwa utagaji wa kuku aina ya Kuroiler na SASSO

Kwa Sasso sijui ila kroiler ni multpurpose, kwa maana wamezalishwa kutokana na kuku wa nyama na kuku wa asili, Ukiwahudumia vizuri wanafaida usiogope comment za watu ambao hajawahi kuwafuga hawa kuku, wewe ingia jaribu, funga kwa lengo la kutotolesha vifaranga hapo ndo utaona faida, niliwahi kuwafunga kipindi fulani na tray ya mayai nilikuwa nauza elfu 15
 

Kwa uzoefu wako wanaanza kutaga wakiwa na miezi mingapi!?
 
Hivi hawa Kuroiler, jike anaweza kupandwa na jogoo wakienyeji na akataga mayai pia vp kuhusu jogoo wa kuroler anaweza kumpanda mtetea wakienyeji na akataga AU NILAZIMA WAPANDANE QENYEWE KWA WENYEWE?
 
Hivi hawa Kuroiler, jike anaweza kupandwa na jogoo wakienyeji na akataga mayai pia vp kuhusu jogoo wa kuroler anaweza kumpanda mtetea wakienyeji na akataga AU NILAZIMA WAPANDANE QENYEWE KWA WENYEWE?
Usijaribu maana vifaranga wanatoka dhaifu sana ,kama unatak kumix mbegu tumia Sasso na kienyeji kuku wako watakuwa wazuri sana
 
Hivi hawa Kuroiler, jike anaweza kupandwa na jogoo wakienyeji na akataga mayai pia vp kuhusu jogoo wa kuroler anaweza kumpanda mtetea wakienyeji na akataga AU NILAZIMA WAPANDANE QENYEWE KWA WENYEWE?
Wanataga vizuri tu na vifaranga wanatoka vizuri kabisa mimi nimewafuga
 
Wanataga vizuri tu na vifaranga wanatoka vizuri kabisa mimi nimewafuga
Nashukuru mkuu je hawa croiler unaweza kuwafuga kama kuku wakienyeji yn ukawaachia wakatoka ndani ya banda wakazurula nawenzao japo ndani ya uzio au wao nindani kwa ndani tu
 
T
 
Hawa ni Dual purpose ni kwa ajili ya nyama na mayai sema sasa wengi huwa hawako balanced yaani wanaegemea sana kwenye nyama kuliko mayai.

Ukitaka kufuga kwa ajili ya mayai fuga Layers kabisa mkuu, chotara hawafai kwa ajili ya mayai
 
Hata mimi nahitaji kujua hili jambo.

Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia anafuga kuku hawa kwa ajili ya kutaga mayai.

Kauli yake hiyo iliniachia maswali kuhusu maslahi yake wakifugwa kwa ajili ya mayai.
Hawa hawafai kwa mayai, mayai fuga layers tu, hawa sana ni kwa nyama,
 
Hawa ni Dual, na wamecrosiwa kwa kuhusishha kuku wa nyama, so wana damu ya kuku wa nyama na kuku wa mayai, sio wazuri kwa mayai
 
Natumae umepata muongozo...




Cc: mahondaw
Hahahaa huu uzi umenikumbusha 2016-2017 nilikuwa nafuga kuku aina ya sasso ndio walikuwa wameingia! hawa kuku sijawahi kuona nilifuga kuku 250 nami nililenga kupata mayai lakini yupo jamaa aliitwa ADAM NYAMANGE mkurugenzi wa mtandao wa kijani kibichi alinitembelea baada ya kuona kwenye mitandao nafuga kuku wakubwa sana alivyofika kuku wangu walikuwa na miezi 5 na walianza kutaga na utagaji wake sio MZURI sana huwa wanaruka Siku lakini wana maumbo makubwa sana! akaniambia kwa mayai hutafanikiwa weka nguvu kwenye kuwahudumia uuze nyama!!
Nilianza kutafuta masoko kuku walikuwa wakubwa sanaa tetea kg 4 nilikuwa na majogoo 2 wenye kilo 5.5 na kwa ladha sijawahi kula kuku watamu kiasi hicho!! kwa ukubwa wa wale kuku nilipata tenda bodi ya mikopo mwenge! na walinunua kuku mmoja sh 35000 mpaka 40000 jogoo wale wawili aliwanunua mzungu mmoja ambaye aliagiziwa kwangu akajitambulisha kuwa anashughulika na kuku wa sasso na chakula cha SILVERLAND alinunua mmoja 60000 na walipelekwa sabasaba!! nisiongope mradi ule niliufurahia kilichonikera nilipotaka vifaranga awamu nyingine sikupata tena baadae nikaona hawapatikani saso f1 nikahamia kwenye kuroiler!

Kuroiler mayai wanataga vizuri sana ila ladha na ukubwa hawajafikia kwa sasso,, hivi nilipumzika kwa kuku naanza mwaka huu!! Sasa niko kwenye nguruwe na mbuzi wa kisasa wa nyama!!

Ufugaji ukizingatia mbegu bora, chakula cha kutosha, mabanda rafiki, chanjo kwa wakati , research ya masoko ,kufuga kwa muendelezo yaani ujibrand haswaa kila wakati wateja wako wasikose bidhaa ufugaji unalipa ila uhamue haswaaa.
 
Nani ana uzoefu na Kenbro?
 
Nani anauzoefu na Kuku Kenbro?
 
Jitahidi ufuge pure layers au pure broilers achana na machotara labda kama una hela za kuchezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…