Naomba kujuzwa utagaji wa kuku aina ya Kuroiler na SASSO

kroiler ni watagaji wazuri sana, changamoto ni soko la mayai. Ukiuza mayai ya kroiler kwa bei kama ya mayai ya layers huwezi pata faida na wateja wengi uswazi watapendelea mayai cheap ya layers. Lakini kama una wateja wako wa mayai ya chotara watako weza kununua kwa sh 12,000 hadi 15,000 kwa trei fuga mwanagu utapata faida.
 
Unawalisha chakula Cha kampuni gani na vip? Unachnganya na pumba au unawapa peke Cha dukani
 
Sawa.
 
Habari za majukumu wanajamvi
Hivi ukiwalisha sasso formula ya broiler kwa miez miwil ya mwanzo wanaweza kufika kg 2 ndani ya miez miwili
 
uzi mzuri, kuna elimu hapa
Ndio mkuu tunahitaji hiyo elimu ili tuweze kufuga ufugaji wa kuku wenye tija kama nchi zilizoendelea sio kufuga kimazoea mathalani ufugaji wa kuku wa kienyeji binafs nauona kama ni ngumu kutengeneza faida kubwa kwani uzalishaji huchukua muda mrefu sana japo sisemi ufugaji wa kuku wa kienyeji ni mbaya hapana huo ni mtazamo wangu tu
 
Asante saana, kweli kuku wa Sasso kwa mayai sio ila kwa nyama wako safi sana. Mimi changamoto ninayokutana nayo kwa kuku hao kwa upande wangu wanaugua saana flue, macho na kuna wakati wanakua walegevu miguuni. nimepambana nao sana ila sijapata utatuzi wa kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…