Naomba kujuzwa uzuri wa hii Noah new shape

Gari ya 12m mwaka 2015 umeiuza 2020... 6m bado unaona ni hasara watu mna moyo aisee.
Kipindi hicho mpaka inaingia road nlitumia 13M na ushee. Pia kumbuka mpaka nikaamua kuiuza ilishaninyonyoa parefu kwenye matengenezo.Niliwahi kuipeleka mpaka kwa wachina, ila baada ya muda kidogo mambo ni yaleyale.
Anyways, kila mtu na bahati yake. Sisemi niliyoyapitia kwenye hizo Noah ni lazima iwe hivyo kwa kila mtumiaji, ndio maana wengine bado wanazitumia. Anaetaka kuzinunua anunue tu, sababu mwisho wa siku kila mtu ana maamuzi binafsi juu ya pesa zake.
Ile 6M sahivi nimeiingiza kwenye kununua mazao mkoani na kuja kuuza hapa jiji la Kunenge. Sina muda mrefu tangu nianze hili, ila so far so good. Pesa inaonekana
 
Comments zetu tusio na magari sasa β€œsio gari kabisa” πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mara nyingi usihesabu gari kama investment hata siku 1 labda iwe gari ya biashara 100% na ina vibali kwa ajili ya biashara.

Usitegemee ununue gari kwa matumizi binafsi halafu uione kama biashara.
 
Kwaio ulikaa na gari miaka 5 uulitaka uliuze kwa kiasi gani ukilinganisha na ulivyolinunua? Pia ungesema mazingira uliyokua ukiishi na kutumia mara kwa mara na service history itapendeza sana mkuu ili tutoe hitimisho zuri
 
Nunua old model liko juu halafu halisumbui chukua liteace Noah au townace Noah ni gari imara Sana baadhi ya maeneo mikoan inatumika Kama hiace kwa sabb ya uimara wake.
 
Fuata ushauri wa wadau hapo juu [emoji115][emoji115][emoji115]
Nunua LiteAce Noah ama TownAce Noah (SR 40/50) au CR 50(manual) . Nimemiliki SR 50 kwa miaka nane, sijawahi kuwa na shida nayo hata kidogo.
Unalitumia kibiashara kusafirisha abiria au unalitumia kwa matumizi ya familia? Hongera umejitaid kulitunza Mana miaka 8 ni mingi .
 
Unalitumia kibiashara kusafirisha abiria au unalitumia kwa matumizi ya familia? Hongera umejitaid kulitunza Mana miaka 8 ni mingi .
Private use, ila limepiga trip mikoa mingi sana mijini na vijijini. Kikubwa, usilinyime service pale linapohitaji, kwa maana ya kwamba usisubiri liharibike kitu kikubwa ndipo ulirekebishe.
 
Private use, ila limepiga trip mikoa mingi sana mijini na vijijini. Kikubwa, usilinyime service pale linapohitaji, kwa maana ya kwamba usisubiri liharibike kitu kikubwa ndipo ulirekebishe.
Uliagiza Ujapan? Na Ulinunua likiwa na km ngapi na mpaka sasa limetembea km ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…