Niliwahi kuandika humu khs hio mazda rx-8,ngoja ni-paste tena hapa.
Tribute to my mazda rx-8.
Nilikua na mazda rx-8 nikaipimp ikawa ya "kitozi"hatariiiii, balaa lake inakula engine oil si mchezo.
Ni cc 1300 tu,yangu ilikua ni manual 6 speed, horsepower inatoa 240,nilikua nikitembea road hakuna cha tezza sijui nini labda subaru baadhi ndo zilikua zinanisumbua tena mostly STI WRX.
Barabarani ina balance balaa(weight distribution) ni 50% kwa 50%(wenye uelewa wa magari wataelewa hii).
Consumption yake ni lita 1 kwa km 6-8 wkt ni cc 1300 tu, kutegemeana na uendeshaji wangu,hahah.
Ikifika km 100,000 engine overhauling inaweza kuhusika,niliiuza ikiwa na km 75,000 kwa mhindi lkn mpk sasa iko barabarani na zaidi ya km 100,000 na inadunda bila matatizo yoyote yale.
So kwenye rotary engine haitakiwi gari asubuh kuiwasha na kuondoka hapohapo unaiacha kwanza inachemka then ndo unaondoka na ukija kuipaki usiizime pia hapohapo. Na ili idumu atleast kila siku lazima uhakikashe gari inakimbizwa(rev)mpk mshale ufike kwenye redline, kwangu ilikua ni rpm 9000 ukifanya hivyo inadumu
Next challenge nataka 1997 Manual mazda rx-7(Najua matatizo ya hio gari lkn ndo hivyo tena naitaka hivyo hivyo)
I'll miss u my mazda rx-8.