Naomba kujuzwa

Naomba kujuzwa

sunshine1

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
539
Reaction score
291
Habari wana JF,
Naomba kuelimishwa hasa kwa wale ambao ni wanasheria je ni taratibu gani zinapaswa kufwatwa ili kumshitaki kiongozi katika mahakama ya kimataifa ya The Hague? Je ni nani mwenye mamlaka au haki yakumshtaki kiongozi kwenye mahakama hii? Napenda kuelemishwa naamini wapo wengine pia watakaofaidika kutokana na michango yetu katika post hii.

Karibuni!
 
Inamaana jamani hamna mtu anayefahamu kuhusu hii issue ya the Hague au mmeamua kupotezea????!!!!!!!!!!
 
Unaonaje ukaenda kuuliza huko huko the hague?
 
Inamaana jamani hamna mtu anayefahamu kuhusu hii issue ya the Hague au mmeamua kupotezea????!!!!!!!!!!

Taratibu zipo na wajuzi wanachambua sasa watafunguka wakiguswa,unaweza uka google pia.Ila ishu ni very complecated nadhani,unaweza kushtakiwa na kesi nzito zenye ushahidi kabisa lakini kama uko poa na wakubwa hamna shida,wakubwa wakikuchoka wala hushtakiwi unauwawa kabisa tena na mahakama za nchi yako! Sadam ni mfano,ya nini the Hague!?? Kwa uhalifu aliofanya Al Bashiri Darfur anatakiwa kuwa madarakani leo?! na nadhani hata kibali cha kumkamata tayari. we acha tu. Si uliskia kivumbi alicho acha Obama Senegal wamemkamata Rais wa zamani tayari.
 
Kama huna lakuchangia unaweza kukaa kimya! Hili ni jukwaa la great thinkers na siyo great tankers! Tulia tu kama hujui usikubali kuonyesha upumbavu wako mbele ya kadamnasi!!!!!!!!!!!!!!!

Unaonaje ukaenda kuuliza huko huko the hague?
 
Nashukuru sana great thinker kwa mchango wako. Nimekuwa najiuliza hili swali sana na nimelileta hapa kwenye jukwaa kwa makusudi kabisa ili watuwanapochangia wa reflect pia. Kila tukiangalia hali ilivyo Tz kwa sasa na ukandamizaji wa wazi unaofanywa na serikal pamoja na vyombo vya usalama tunapata picha kuwa hii si haki. Lakini je nani atakayeiwajibisha serikali ambayo pia imeshika dola? Mara nyingi utasikia watz wakisema ngoja tu hawa viongzi wetu wasubiri the Hague. Je tunajua nani mwenye mamlaka wakuwapeleka huko? Je tunajua taratibu na vigezo vyakuwashitaki The Hague? Kama hatujui tufanye nini basi hasa hali inapozidi kuwa mbaya na ukandamizaji kuongezeka siku hadi siku? Tusiwe tu wepesi wakuepuka majukumu kwakutoa majibu mepesi yakusema tusubiri The hague iwawajibishe viongozi wetu. We must also think of the alternatives to liberate ourselves!

Taratibu zipo na wajuzi wanachambua sasa watafunguka wakiguswa,unaweza uka google pia.Ila ishu ni very complecated nadhani,unaweza kushtakiwa na kesi nzito zenye ushahidi kabisa lakini kama uko poa na wakubwa hamna shida,wakubwa wakikuchoka wala hushtakiwi unauwawa kabisa tena na mahakama za nchi yako! Sadam ni mfano,ya nini the Hague!?? Kwa uhalifu aliofanya Al Bashiri Darfur anatakiwa kuwa madarakani leo?! na nadhani hata kibali cha kumkamata tayari. we acha tu. Si uliskia kivumbi alicho acha Obama Senegal wamemkamata Rais wa zamani tayari.
 
Habari wana JF,
Naomba kuelimishwa hasa kwa wale ambao ni wanasheria je ni taratibu gani zinapaswa kufwatwa ili kumshitaki kiongozi katika mahakama ya kimataifa ya The Hague? Je ni nani mwenye mamlaka au haki yakumshtaki kiongozi kwenye mahakama hii? Napenda kuelemishwa naamini wapo wengine pia watakaofaidika kutokana na michango yetu katika post hii.

Karibuni!
Ni hivi hiyo ICC inaweza kuinstitute proceedings kwa njia kuu 3..1 personal initiative of the prosecutor..wa ICC mfano ni Kesi ya Ocampo six iliyo wahusu akina uhuru kenyata etc 2. Government ya hiyo nchi..mfano museveni aliombaga kumshitaki sijui jamaa gani yule 3 njia ya mwisho ni ya kupitia kwa UN security council resolution mfano kilicho tokea libya security council ndo ilipitisha azimio hilo kama unapenda jua zaidi download rome statute 1998..over..!!!
 
Thanks mkuu Lyamber!

Kwa kuongezea alipomalizia Mhe. Lyamber kabla hujafikiria kufungua kesi yoyote ni vyema ukajihakikishia kuwa una stahili ya kimaslahi katika kesi hiyo kisheria inaitwa "LOCUS STAND" kwa maana kama itaonekana unakosa locus stand kesi hiyo haitakuwa na "Merit" na hivyo mahakama itakataa kuisikiliza.
 
an individual person hawezi kufungua kesi the Hague, the only thing an individual person can do is to spread awareness ili labda, mashirika ya kimataifa yasikie, na habari zaidi zisambae labda state parties to the Rome statute of International criminal court wasikie na kupeleka issue the hague, au security council wasikie wakakaa na kuamua jambo liende kule, au pengine Fatou bensuda mwenyewe akasikia akaanzisha uchunguzi yeye mwenyewe suo motto.

kwa kifupi ni kwamba, the ili kesi ianze kuchunguzwa hadi kusikilizwa na the hague, zipo njia tatu tu ambazo suala linaweza kufikishwa pale, na zo ni
  1. state parties(nchi zilizotia saini mkataba wa Roma) wapeleke jambo hilo kwa prosecutor to move him/her to initiate investigation
  2. security council of the UN wanaweza kukaa wakaamua jambo lipelekwe kwa prosecutor aanzishe uchunguzi
  3. prosecutor mwenyewe (kwasasa ni Fatou bensuda, zamani alikuwa ocampo) anaweza kuanzisha uchunguzi hadi kushitaki bila hao hapo juu.
utaona kuwa, watu binafsi hawana access kwenda kupeleka jambo kule moja kwa moja, labda kwa kupitia milango ya nyuma sana. nimeongea kifupi sana.

kwa mambo mengine, bofya hapa www.sheriakwakishwahili.blogspot.com

View attachment 102852

View attachment 102852

View attachment 102853View attachment 102853View attachment 102853View attachment 102853
 
Back
Top Bottom