Ngugu leviz, kwa niaba ya wanaJF sisi hatujambo sijui upande wako wewe? naomba niende moja kwa moja kwenye ombi lako la kufahamu namna ya kufungua kampuni ya utalii.
ILI KUJIBU SWALI LAKO naomba kwanza nikukmbushe ama kukufahamisha kuwa UTALII imeundwa na sectors hizi
A) TRANSPORTATION
Hapa ni usafirishaji wa watalii kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwa usafiri vyombo vya nchi kavu kama magari, pia kwa usafri wa angani, na majini.
B) ACCOMODATION
Malazi kwa upande wangu huwa naamini ni kiini cha utalii kwani hapa ndipo unaipta hospitality yenyewe tena pure kabsaa kwenye utalii. katika kipengele hiki unaweza kuwekeza kwenye HOTEL, CAMPING, LOUNGE, LODGE,BED & BREAKFAST na aina nyingine za malazi.
C)FOOD AND BEVARAGE
Hapa utaweza kumudumia mtalii katika hatua zake zote atakazokuwa ana experiace utalii ka nyanja zote, katika kipengele hiki kuna RESTAURANT, BARS & CAFES, CATERING and NIGTH CLUBS hapa pia kuna hospitality ya kipekee sana.
D)ENTARTAIMENT
Wengi wa watalii hufuata aina fulani ya burudania ambazo kwa namna moja ama nyingne hazipatikani katika mazingira ya kwao au zina vionjo na ladha tofauti mfano ni wilderberst migration in northen serengeti aina hii ya burudani huatikana serengeti tuu dunia nzima, pia fikiria kuhusu vyakula vya asili na tamaduni mbali mbali duniani hii ni mifano ya aina za burudani na vionjo vinavyowafanya watalii kusafiri. hapa kuna vipengele kama CASINO, TOURIST INFORMATION, SHOPING (kama maduka ya vinyago),na TOUR GUIDES AND TOURS.
Ndugu Leviz Bila shaka wewe unafikiria upande wa TOUR GUIDES AND TOURS.
Kama jibu ni ndiyo basi nianze kwa kujibu kipengele kimoja baada ya kingine.
1. USAJILI WA KAMPUNI YA UTALII
Kabla ya usajili wa kampuni ya utalii ni vyema ukaandaa kwanza katiba ya kampuni yako, na ukajua ni aina gani ya umiliki wa kampuni utachagua kama vile sherehollder, patrernship, and others, fuata hatua hizi ili uweze kusajili kampuni yako
1)Kusanya taarifa za wahusika | wahusika ni wamiliki wa kampuni kama vile wanahisa |
2)Andaa nyaraka za usajili | declaration of complience, article of asosiation |
3)Jaza maombi kwenye website ya BRELA ORS | Jaza taarifa ulizokusanya kwa mtiririko uliopangwa na BRELA ORS |
4)Download nyaraka toka brela | baada ya kujaza maombi utaweza kudaonload form |
5)UPLOAD nyaraka kwenye brela | nyaraka hizi ni zile ulizoandaa kwenye hatua ya pili na ulizodanload kwenye hatua ya 4 |
6)Lipia control number | baada ya kuapload kila kitu utapatiwa control number ya kulipia |
7)subiri maombi yafanyiwe kazi | Maombi yatafanyiwa kazi na utapokea ujumbe kwa njia ya email |
8)Pakua cheti toka brela | |
9)Omba TIN | |
10)Omba lesen | |
2.VIGEZO ILI UWEZE KUSAJI LIKAMPUNI
wamiliki, vitambulisho vya taifa, katiba ya kampuni, na jina la kampuni lisilofanana na kampuni nyingine.
3.MASOKO YA WATALII NA WAPI PAKUYAPATA
jisajili kwenye tourism organization kama vile TATO, TALA pia shiriki katika maonesho ya utalii yanayokutanisha kampuni zote za utalii na washirika wake. pia unaweza kuweka ama kutafuta tourism agent wa kukufanyia marketing promotion nje na ndani ya nchi.
3.WAFANYAKAZI WA MUHIMU
Kwenye utalii naona kila idara ni ya muhimu apo wewe utaangalia idadi ya wafanyakazi uibalance vp, mfano mtu anaweza akawa asigned kufanya kazi zaid ya mbili kama vile apo apo ni dereva na tour guide. hili ma HR wanaweza wakakupa muongozo zaid.
LUGHA ZA MUHIMU KWA WAFANYAKAZI WAKO
Hapa inategemea na wewe unatakuwa umijibrand ama market yako kubwa ya watalii itakuwa ni kutoka sehemu gani ya uso wa dunia ila ni vyema ukawa na guides wanaofahamu kuzungumza lugha kama vile french, spanish,na kiingereza, kwani hizi ni lugha ambazo zina wazungumzaji wengi.
Nawasailisha nikiwa site apa namsaidia fundi kujenga.
AHSANTE