Naomba kupata uzoefu kwa wakulima wa dragon fruit!

Naomba kupata uzoefu kwa wakulima wa dragon fruit!

ghalim7090

Member
Joined
Sep 25, 2026
Posts
5
Reaction score
7
Habari Wana familia jamii forum!

Nimekuwa najihusisha na kilimo cha dragon fruit kwa miaka kama 4 sasa japo siyo kwa kiwango kikubwa.

Nimeona kuna mambo mengi ambayo ni muhimu kuyafaham juu ya kilimo hiki hasa magonjwa, wadudu wasumbufu na waharibifu hasa kono kono, pia kuhusu self-pollination, cross-pollination na aina zinazohitaji pollinizer.

Pia nimeona mavuno yanaweza kutofautiana kulingana na aina, hivyo ningependa kupata uzoefu wa wakulima wengine kuhusu aina walizolima, uchavushaji, changamoto walizokutana nazo na namna walivyozitatua.

Nimetaja pia suala la miche kwa sababu aina unayochagua inaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwenye uchavushaji na mavuno.
Lakini zaidi ya yote ningependa tushirikishane uzoefu ili tujifunze kutoka kwa kila mmoja.

Kwa waliowahi kulima na kuvuna, kwa wastani mmeweza kupata mavuno kiasi gani kwa mmea mmoja au kwa ekari, na ni aina gani imewapa mavuno hayo? Pia, mmeona tofauti gani ya mavuno kati ya mimea inayofanya self-pollination na ile inayohitaji cross-pollination?
 
Wewe upo sehemu gani, na unaweza kwenda masasi?
 
Mkuu tupia picha za shamba lako pia

Sawa.
Kama nilivyosema nafanya lakini kwa kiasi kidogo kwa sasa ndiyo nataka kuweka kwa kiasi kikubwa maana miche ninayo ya kutosha.
Kuna mashina ambayo niliweka moja moja sehem tofauti ambayo ndiyo nilizalishia miche mipya nitatafuta picha zake nitaziweka pia
 
Habari Wana familia jamii forum!

Nimekuwa najihusisha na kilimo cha dragon fruit kwa miaka kama 4 sasa japo siyo kwa kiwango kikubwa.

Nimeona kuna mambo mengi ambayo ni muhimu kuyafaham juu ya kilimo hiki hasa magonjwa, wadudu wasumbufu na waharibifu hasa kono kono, pia kuhusu self-pollination, cross-pollination na aina zinazohitaji pollinizer.

Pia nimeona mavuno yanaweza kutofautiana kulingana na aina, hivyo ningependa kupata uzoefu wa wakulima wengine kuhusu aina walizolima, uchavushaji, changamoto walizokutana nazo na namna walivyozitatua.

Nimetaja pia suala la miche kwa sababu aina unayochagua inaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwenye uchavushaji na mavuno.
Lakini zaidi ya yote ningependa tushirikishane uzoefu ili tujifunze kutoka kwa kila mmoja.

Kwa waliowahi kulima na kuvuna, kwa wastani mmeweza kupata mavuno kiasi gani kwa mmea mmoja au kwa ekari, na ni aina gani imewapa mavuno hayo? Pia, mmeona tofauti gani ya mavuno kati ya mimea inayofanya self-pollination na ile inayohitaji cross-pollination?
Kabla hujalima lazima utambue yafuatayo.
1. Hali ya hewa, Dragon zinataka ukanda wenye jua kari la mda mrefusana.

2. Maji, umwagiliaji ni muhimu sana wakati wa kiangazi hakikisha maji yapo.

3. Aina za Dragon, aina ziko zaidi ya 50 huko, na sio zote ni nzuri kuna mabazo taste yake tu mtu harudii tena kula ama zina taste mbaya sana.

4.Soko, soko hapa ni kwenye miji mitatu tu, Dar, Arusha na Zanzibar,huko kwingine sio kabisa na kwenye hii miji mikubwa nimetaja kwa sbabau ina Foreigners wengi dana na watu pia walio toka sana huko Duniani.

5. Msimu upo yes, inaanza maua miezi hii ya mwezi wa 11 na kuanzia mwezi wa 12 matunda yanaanza hadimwakani mwezi wa 6 huko.

7.Mavuno, under good management mti mmoja unaweza zaa matunda hadi 40 hapo ni maxim ila mara nyingi inazaa chini ya hapo.

Bei zake kwa sasa zimeshuka sio kama zamani huo, bei inaenda hadi 3000 hadi 5000 kulingana na size ya tunda.

8. Dragon ni delicate sana kwenye swala la transport ingawa tunda lake lina life span nzuri hata kuzidi embe.

9. Hekari 1 inabeba nguzo 500 sawa na mashina 2000

Shinda 2000 maana yake ni shina 4 kwa kila nguzo moja.

Alla ina all Dragon ni matunda ya afya zaidi kuliko utamu wake ama taste yake, kama watu sio afya sensitive haya sio matunda yao kabisa ama kwa wale watu wa taste sensitive pia sio matunda yao.
 
Back
Top Bottom