Naomba kupewa elimu juu ya Mbao za kuezekea Nyumba

Hii kweli ni elimu tosha. Lakini sisi watu wa mikoani tutajuaje kuwa hizi mbao zimetoka sao hill??? Maana wafanya biashara ni wajanja wanaweza kukuambia ni mbao imetoka Sao hil kumbe imetoka Ukerewe [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nje ya mada ,Kwa wajuzi bei ya mbao ilivyochangamka na changamoto za kuliwa na wadudu sio wakati muafaka wa kutumia chuma badala ya mbao kwenye kupaua?
Chuma ni gharama sana
 
Sina uhakika sana kama zinapatikana sabasaba kwasababu mimi sikuzinunulia huko. Ilikua 2017 bei yake ilikua nafuu kidogo kulinganisha na mbao za Iringa. Sikumbuki bei exactly ila zilikua na unafuu wa shilingi 400 hadi 700 kwa mbao kulinganisha na za Iringa. Tembelea masoko ya mbao ufanye utafiti kabla ya kufanya manunuzi.
Dawa nilinunua mwenyewe kwenye maduka ya pembejeo za kilimo dumu la lita5 nimeisahau jina, hazikupakwa bali zililowekwa kwenye hiyo dawa.
 
Mbao za sao hill zipo aina kadhaa kutokana na upasuaji mbao, za kwanza ni za kutoka kiwanda kilichokuwa cha serikali caha sao hill , hizi utazijua kwa jinsi zilivyochanwa kwa umaridadi na ni ghali pia , aina ya pili ni mbao ambazo zimachanwa na watu binafsi hizi mara nyingi zinakuwa rough kidogo . Sao hill huwa anauza misitu kwa watu binafsi pia yeye zake anachana kwa kiwango cha juu ndo maana anauza ghali
 
Leo nimekutana na hili swala la mbao zinalowekwa kwenye dawa sasa katika uchunguzi wangu wa chini kwa chini bila wahusika kujua nikafanikiwa kupata kopo la hiyo wanayoita dawa ya mbao nikabaki nashangaa tuu. Je food color ni dawa ya mbao????? Kikopo hicho nime attach
Ndio wanasema mbao zime tritiwa
 
Mi nadhani ujenzi unaofata nitatumia chuma badala ya mbao! Kuna ujanja mwingi sana kwenye mbao na bado ni gharama na wala hazikai muda unaanza kusikia wadudu juu ya dari.
 
Mi nadhani ujenzi unaofata nitatumia chuma badala ya mbao! Kuna ujanja mwingi sana kwenye mbao na bado ni gharama na wala hazikai muda unaanza kusikia wadudu juu ya dari.
Tufanye utafiti wandugu tunapigwa sana yani food color ina treat mbao 🙄
 
Kumbe kuna mbao za kuchemshwa na kukaangwa na Hamsemi😅😅
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna watu ni wezi Sana. Bora kutumia oil ama wewe mwenyewe kwenda duka la agrovet kununua dawa.
Mtuambie hizo dawa za agrovet zinaitwaje?
 
Tumia mbao za mlingoti.. Huna haja ya kuweka dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…