* Naamini unataka kuanzisha ONLINE TV na sio YOUTUBE CHANNEL.
Ila kama unataka kuanzisha Youtube Channel, ni rahisi;
1. JINSI YA KUFUNGUA: Sign up kwa kutumia barua pepe yako ya Gmail.
*Kisha kalipie leseni TCRA.
2. JINSI YA KUPATA PESA:
- ADSENSE: Unahitaji kuwa na subscribers 1,000 na view time ya masaa 4,000 ndani ya miezi12 kabla hawakuwezesha ku-monetize video zako.
- UZA BIDHAA, 'MERCHANDISE' na HUDUMA.
Wasome watazamaji wako wanataka nini na kisha wauzie kitu cha thamani kwao.
- FANYA AFFILIATE MARKETING.
- INGIA DEALS NA BRANDS KUBWA NA SPONSORSHIPS.
- CROWDFUNDING n.k
3. VIFAA: Camera HD, mic, Lighting system, na software za ku-edit video & picha.
4. WATU: Unahitaji watu kukusaidia kurekodi video, ku-edit na ku-manage mitandao ya kijamii kama huwezi kuvifanya hivi vitu wewe mwenyewe.
5. MAUDHUI: Kuna chaneli nyingi sana hivi sasa - unahitaji kuwa mbunifu sana ili kuwavutia watazamaji.
Lakini kama unataka kuanzisha online TV;
NAMNA YA KUANZISHA INTERNET/ ONLINE TV.
*Assuming kwamba una mtaji mdogo na kwahiyo utaanza ukiwa jeshi la mtu mmoja. Na si lazima ufuate mfululizo kama nilioupanga mimi.
HATUA YA 0: Kwa 'heshima na taazima'(Taadhima) nenda kawaone TCRA kwanza.
Mjanja huwa anatatua matatizo, mwenye busara huwa anayaepuka matatizo. Unataka mjanja au mwenye busara? Ukifika kwa hawa jamaa waambie kusudio lako la kuanzisha Online TV - watakupa muongozo rasmi, vigezo na masharti. Labda kama wewe huishi hapa kwetu, Tanzania.
HATUA YA 1: Liweke vizuri wazo lako ili ujue wapi unakotaka kuelekea.
Utajuaje kama umeliweka vizuri? Well, kama huwezi kulielezea kwa sentensi moja au mbili likaeleweka basi bado hujajua unachokitaka. Jiulize maswali haya;
- Unataka kupata nini kutokana na hiyo online TV yako?
- Ni maudhui gani unataka kuyatoa?
- Yapi yatakiwa masaa yako ya kazi?
- Ni wakati gani utakuwa live na muda gani utarusha vipindi ambavyo ni pre-recorded?
- Tengeneza ratiba ya matukio na topics.
HATUA YA 2: Nunua domain.
Nashauri ununue 'domain name' mahsusi kwaajili ya online TV tu. Domain za 'Dot TV (.tv)' zimekuwa maarufu sana kwa masuala ya TV. Lakini; unachotakiwa kufahamu ni kuwa .tv haiwakilishi 'television'. Kiuhalisia .tv ni extension ya Tuvalu, taifa lililopo katika visiwa vya Polynesia.
HATUA YA 3: Ajiri watu - tengeneza timu kwaajili ya ku-design na ku-code website.
- Inatakiwa kuwa kama website zingine. Utofauti ni kuwa; katikati ya website weka TV kubwa inayo-stream video au matangazo mubashara (live).
- Weka sehemu za matangazo ya wadhamini wako.
- Weka sehemu ambayo watazamaji wako wanaweza ku-browse bidhaa na huduma zako, kufahamu zaidi kuhusu wewe, kuwasiliana na wewe na vitu vingine vya namna hiyo.
- Hakikisha una-update website yako mara kwa mara ili kubadilisha matangazo n.k.
HATUA YA 4: Tengeneza eneo la kurekodia.
Naamini utakuwa unafanya vipindi aina zote; yaani pre-recorded na live videos, kwahiyo ni muhimu ukawa na sehemu maalumu ya kurekodia ambayo imepambwa inavyotatikana na ina vifaa vyote muhimu kwaajili ya kuhakikisha video zako zinakuwa na ubora.
HATUA YA 5: Nunua vifaa kwaajili ya video recording video na live broadcasting.
Unaweza kupata hivi vifaa vyote kwa chini ya TZS 5,000,000/=
- HD camera ni lazima.
- Vifaa vya audio: microphone, headphone, 'clipped microphone', au unaweza kuamua ukanunua vyote 'wireless'.
- Vifaa kwaajili ya lighting: Chagua vifaa bora kwa utashi wako.
- 'Green screens'. (Hizi zinasaidia kurahisisha kazi ya ku-edit video na picha za kawaida.)
- 'Teleprompter'; Hii utaihitaji ikiwa tu utataka kuendesha vipindi vyako kwa kutumia 'script'.
- Unganisha camera yako na computer yako, na jiandae kwenda live!... Camera -check ,.... lights - check.... voice - check.... tunaenda hewani baada ya sekunde 5 - 4 - 3 - 2 -..
HATUA YA 6: Tafuta host mzuri wa website yako ambae anaweza ku-handle bandwidth na video streaming mfululizo.
*Kama wapo humu watajitokeza, au la tafuta mtandaoni utawapata.
HATUA YA 7: Anza kurekodi videos ambazo utaziweka katika station yako.
Si lazima uwe na video nyingi au ndefu ili uanze. Unaweza kuanza na video moja au mbili - cha muhimu ni kuanza. Fuata muongozo uliojiandalia wewe mwenyewe kuhusu maudhui utakayoyatoa ukiwa live na yale utakayorekodi.
HATUA YA 8: Kumbuka si lazima uwe na maudhui ya kutosha kuruka 24/7.
- Unaweza ukapiga masaa manne ya maudhui ambayo ni pre-recorded kila siku, masaa mawili ya kwenda live na matangazo unachanganya humo humo.
- Rudia hayo maudhui yaliyoruka live kwa masaa sita.
- Masaa mengine 12 yaliyobaki kuwa mbunifu - weka mziki au chochote unachoona kinawafaa watazamaji wako.
Si nyakati zote utapata watazamaji wa kutosha. Hivyo ni vizuri kujua 'peak hours' zako. Hakuna haja ya kurusha kipindi endapo huna watazamaji.
HATUA YA 9: Host baadhi ya matukio live.
Live events ni njia nzuri ya kuvutia watazamaji. Utofauti ni kuwa utakuwa una-host tukio kwenye website yako mwenyewe.
HATUA YA 10: Promote chaneli yako kila mahali.
Na ninaposema kila mahali, namaanisha kila mahali.
- Weka link kwenye Website, kwenye mitandao ya kijamii mpaka kwenye sms za watu ukiweza!
- Toa 'taarifa kwa vyombo vya habari' za kutosha. Kuwa msumbufu, acha masihara!
- Fanya 'partnership' na watu wengine kwa malipo ya 'free advertising'.
HATUA YA 11: Teka mji, kuwa mfalme wa online TV!
Kadiri TV yako inavyozidi kuwa maarufu - anza kuongeza tuvitu vitu na fursa za kupiga hela;
- Matangazo (Paid advertising).
- Manbango kwenye website yako.
- Tangaza bidhaa na huduma zako mwenyewe.
- Andaa maudhui yaliyodhaminiwa (Sponsored contents).
- Usiogope - ita watu wazito kwenye interviews zako. Nani ajuaye, labda unaweza kuja kuwa Salama Jabir au Milard Ayo ajaye!
Kisha anza kuajiri kadiri ya mahitaji yako; endapo unahitaji foot soldiers wa kuwinda matukio mtaani au unataka co-hosts, au unataka timu ya production, au unataka social media managers, au unataka script writers, au unataka 'wahariri', au unataka business managers n.k. Angalau ifahamike kuwa idadi ya watu na aina ya watu unaowahitaji inategemea na malengo, mahitaji halisi na bajeti yako.
Ruksa kunikosoa. Naomba kuwasilisha.