Naomba kusaidiwa kuondokana na suicidal mindset

Naomba kusaidiwa kuondokana na suicidal mindset

Pole sana mkuu.. Nichek inbox nikuelekeze jinsi ya kupata tiba.. You will be fine...
 
surrender your life to Jesus that is only solution
 
Maisha ni magumu, ndio, ila ni njia ya kila mtu kutaabika ili kufanikiwa. Usikate tamaa, Muombe Muumba wako akusimamie, washirikishe na uwe karibu na ndugu zako wa karibu, Mama na wadogo zako hizo fikra zinazokukabili. Pia ujue wewe na ndugu zako kwa pamoja ndio mtakaojikwamua katika hali yoyote mliyomo, na kuiboresha. Usitegemee misaada hata kama umeahidiwa, weka juhudi zenu wenyewe, na ikitokea kuna msaada basi ni wa kuongezea tu katika juhudi zenu. Usiwaache nduguzo katika ukiwa.
 
Dawa ya hiyo kitu ni simple sanaaa..... Nenda hospital tembea wodini tembea usiku pande za buguluni tandale uswazi uswazi nenda vituo vya watoto yatima nenda sehemu zozote unazojua watu wana shida ukifika ukiona halihalisi hutafikilia kujiua tena me naamini........
 
Habari wana Jukwaa,

mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25,nimesoma mpaka kidato cha sita lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri.Mwaka niliofanya mtihani ni 2014.

Na baada ya matokeo kwenda mrama nilijitahidi kufanya kazi za hapa na pale ili nikusanye kiasi cha fedha kitakachoniwezesha kujiunga na vyuo vya kati.

Bahati mbaya sana pesa niliyoipata iliishia kuhudumia familia yangu(mimi,wadogo zangu na mama yangu),baba yupo na maisha yake pamoja na ndugu wengine ambao ni half brothers!

Kaka zangu(Half brothers) wamesoma kiasi chake na walikuwa wakitoa ahadi za kunisaidia kusoma lakini mwisho wa siku wanashindwa kutekeleza.

Hivyo nimekuwa nikiishi maisha magumu sana yenye misukosuko sana.


Lakini kuna jambo si jema lilianza mwezi desemba mwaka jana ambalo ni kujiwa na fikra mbaya kichwani zinazonishawishi kujiua kwa kujitupa mbele ya gari au kwa vitu vya ncha kali.


Hali hii ilianza mara baada ya tatizo la kichwa kuuma upande mmoja(migraines) kwisha.
Nimejaribu kulazimisha ubongo ufikirie mengine lakini wapi!naomba wataalam mliopo humu jukwaani mnisaidie nini hasa tatizo langu na nifanye nini kuondokana nalo,


Asante na nawasilisha!

MTWIKE YESU FADHAA ZAKO ZOTE


Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; HUKU MKIMTWIKA YEYE FADHAA ZENU ZOTE, KWA MAANA YEYE HUJISHUGHULISHA SANA KWA MAMBO YENU’ [HASHTAG]#1PETRO[/HASHTAG] 5:6,7

Bwana Yesu hushughulika na kila aina ya fadhaa za mwanadamu. Imeandikwa “Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa KILA namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya” # Mathayo 4:23,24

Yesu habagui tatizo. Wewe mpelekee tu. Yuko tayari kulishughulikia. Ukiamua kukaa na hilo tatizo linalokusumbua shauri yako. Yeye yuko tayari kukusaidia. TATIZO

YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU, KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.
Kwa maombezi au ushauri au unajisikia ndani ya moyo wako unataka kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako ili alete mabadiliko ndani ya maisha yako ya kila siku au unataka kutumiwa mafundisho kila siku kwa whatsapp

basi wasiliana kwa namba hii bila kusahau kusahau kutupa majina yako

0758 443 873
 
Pole sana.hiyo ni psychological disorder. Aidha nenda hospitali ukatibiwe kabla hujazidi kuchizi au kama unamsuli ngangamala na maisha,jitume,jiamini,jipende na utatoka tu.put in mind like kufa ni kushindwa weka nia ya kuishi na kufanikiwa ili wanaokudharau waaibike.Ktk hiyo nia yako muombe Mungu.
 
Pole sana.hiyo ni psychological disorder. Aidha nenda hospitali ukatibiwe kabla hujazidi kuchizi au kama unamsuli ngangamala na maisha,jitume,jiamini,jipende na utatoka tu.put in mind like kufa ni kushindwa weka nia ya kuishi na kufanikiwa ili wanaokudharau waaibike.Ktk hiyo nia yako muombe Mungu.
Asante sana
 
Nenda Ocean Road pale katembelee wagonjwa siku moja pita ward zote tu randomly af jiulize kati ya wewe na wao nani ana maisha ya misukosuko
 
Back
Top Bottom