Naomba kusomeshwa kwa mkataba

NATIONALISM

Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
24
Reaction score
1
Ndugu wanajamvi hili, ninaleta hili kwenu ninaomba atakaye guswa na hili na uwezo wa kunilipia nusu ya ada ya chuo yaani laki tano kwa mwaka kwa mkataba maalumu nipo tayari.

Ahsante.

 
Ndg wanajamvi hili,ninaleta hili kwenu ninaomba atakaye guswa na hili na uwezo wa kunilipia nusu ya ada ya chuo yaani laki tano kwa mwaka kwa mkataba maalumu nipo tayari.
Ahsante

NATIONALISM unapotaka kusaidiwa na watu unatakiwa utoe maelezo ya kutosha ili watu waguswe na maelezo yako
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hii iwe changamoto kwa Uongozi wa JF, uone haja ya kuweka jukwaa maalumu ambapo wahitaji kama hawa wanaweza kukutanishwa na Wafadhili.

Ifike wakati sasa tupunguze japo kidogo kuchangia sherehe kama wenzetu wa Kenya. Tunahitaji elimu kwa vijana wetu, nani ajuaye huyu mleta uzi anaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwa Taifa.
 
Pole nationalosm wewe ni jinsia gani, na una umri gani, na una ujuzi gani na ni chuo gani unataka kusoma na katika level ipi.

Ukijibu hili utatoa muongozo.
 
pole nationalosm wewe ni jinsia gani,na una umri gani,na una ujuzi gani na ni chuo gani unataka kusoma na katika level ipi
ukijibu hili utatoa muongozo


Umri: 27

Sex: M

Chuo: SAUTI - Mwanza

Course: BAED

Kwa bahati sana,sina hatima kama nitamaliza chuo ambapo ni historia kubwa tangu huko nyuma mpaka nafika hapa,offcourse kwa nguvu za mungu,lakini naona hapa nitashindwa , mpaka sasa nimezuiliwa kufanya (university exam), nikaamua kuandika barua ya kuomba special exam,tatizo je?

nitaipata hiyo au itakuwa ndo mwisho wa ndoto zangu, nimeappeal lakini mpaka sasa hamna majibu, watanzania, najua humu kuna viongozi sikilizeni vilio vya watanzania wenzenu,mimi ni maskini wa kipato ila si maskini wa akili.nafikia muda najuta kwanini nimezaliwa familia maskini ambapo unakuwa ni msalaba au kilio kwangu watoto.

Naomba yeyote atakayekuwa yuko tayari, hata kwa mkataba baada ya kumaliza chuo mimi nitapiga kazi narejesha mdogo mdogo,kwa sisi saut kwa mwaka ni milioni moja na laki nne,tatizo lingine ndg aliyekuwa ananipiga tafu amefariki mwaka jana kwa ajali ya gari.hapa nilipo sijui mara ya mwisho nilikula lini,siku nikipata chakula namshukru mungu,ikipita basi.

Najua watanzania tunazidiana uwezo ndo maana naandika haya.

Nasuria maoni yenu,ukimsaidia maskini mungu atakusaidia mara dufu.
 
nimejaribu kuongea na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini lakini hamna hatima ya matatizo yangu.
 
Pole mdogo wangu... Kwa wenye kuweza watakuja muombe mola.

Mkuu hongera hata kwa kufika apo. Last alternative yooote yakigoma hairisha mwaka pata kibarua mwakani malizia. Binafsi sina uwezo ningekusaidia, pia usikate tamaa , mko wengi mno ila ndio serikali na jamii imewatenga.

Binafsi kuna mdada babake alimkataa mama yake alikuwa mwalimu akaachishwa kazi na mme kamzalisha alaf kamfukuza, mtoto kakwama form 4....

Nikamchukua akakaa kwangu, tukakubaliana aende certificate, alipomaliza , akaenda diploma ...kamaliza mwaka jana ili sasa aombe mkopo aende chuo. Tuliapply akaomba SUA then TCU wakampanga ifm , mkopo status ni BUDGET EXHAUSTED.....

Kwa kweli imeniuma sana na uwezo wangu ni mdogo na pia wadogo zangu nawasaidia mm na ikumbukwe hatuna undugu wowote na uyu binti, ni kuwa tu alikuwa bright na akaja kunieleza nikaona nijikunje. Kwa sasa yupo tu apa nyumbani.

Kwa kifupi hauko peke yako ila yachukulie kama maisha na usimkashifu mungu kwa kukupa hali iyo.

Ipo siku utayasahau ayo mateso. " YANA MWISHO AYA".

Pole kijana.
 
NATIONALISM

i wish to help you ila kazi yangu ni ya kipato cha chini na nasoma tena degr ya pili kwa hali ya kimagumashi tu yaani ila ndugu yangu mi nina ushauri kidogo ungeomba mtaji utakaokuwezesha kumiliki kabiashara huku unasoma ambako hakatakubana.

kwa mfano biashara ya Mpesa ambayo utaifanya ukiwa shule

MAANA KUOMBA ELA KILA SIKU NI KARAA AMBAYO HAKUNA AIPENDAE PIA UNAEZA UKAWA WAKALA LETS SAY WA KUSAMBAZA TSHIRT UKO CHUONI,

ukaomba uwakala sehem mbalimbali
 
Last edited by a moderator:
Nenda kanisani kwenu au msikitin,omba waumin wakufanyie harambee.nimeshuhudia jamaa mmoja wa Mzumbe amefanikiwa kwa njia hyo.
 
Hivi hawa mabilionea wa jf bado hawajajitokeza kukupa msaada.maana humu ndani kila mtu ni tajiri
 
nimejaribu kuongea na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini lakini hamna hatima ya matatizo yangu.

Pole mkuu.

Hawa watu ni wanafiki kuwahi kutokea... Wanakusanya kingi sana kutoka kwa masikini na hawarudishi HATA KIDOGO!

Vipi ndugu hawapo wa kusaidia bila masharti?
 
Pole mkuu.

Hawa watu ni wanafiki kuwahi kutokea... Wanakusanya kingi sana kutoka kwa masikini na hawarudishi HATA KIDOGO!

Vipi ndugu hawapo wa kusaidia bila masharti?

Bado sijafanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…