NATIONALISM
Member
- Jul 10, 2013
- 24
- 1
Ndugu wanajamvi hili, ninaleta hili kwenu ninaomba atakaye guswa na hili na uwezo wa kunilipia nusu ya ada ya chuo yaani laki tano kwa mwaka kwa mkataba maalumu nipo tayari.
Ahsante.
Ahsante.
Umri: 27
Sex: M
Chuo: SAUTI - Mwanza
Course: BAED
Kwa bahati sana,sina hatima kama nitamaliza chuo ambapo ni historia kubwa tangu huko nyuma mpaka nafika hapa,offcourse kwa nguvu za mungu,lakini naona hapa nitashindwa , mpaka sasa nimezuiliwa kufanya (university exam), nikaamua kuandika barua ya kuomba special exam,tatizo je?
nitaipata hiyo au itakuwa ndo mwisho wa ndoto zangu, nimeappeal lakini mpaka sasa hamna majibu, watanzania, najua humu kuna viongozi sikilizeni vilio vya watanzania wenzenu,mimi ni maskini wa kipato ila si maskini wa akili.nafikia muda najuta kwanini nimezaliwa familia maskini ambapo unakuwa ni msalaba au kilio kwangu watoto.
Naomba yeyote atakayekuwa yuko tayari, hata kwa mkataba baada ya kumaliza chuo mimi nitapiga kazi narejesha mdogo mdogo,kwa sisi saut kwa mwaka ni milioni moja na laki nne,tatizo lingine ndg aliyekuwa ananipiga tafu amefariki mwaka jana kwa ajali ya gari.hapa nilipo sijui mara ya mwisho nilikula lini,siku nikipata chakula namshukru mungu,ikipita basi.
Najua watanzania tunazidiana uwezo ndo maana naandika haya.
Nasuria maoni yenu,ukimsaidia maskini mungu atakusaidia mara dufu.