Naomba kuuliza hili kwa niaba ya kina mama(wanawake)

Carla

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
398
Reaction score
331
Ni kitu ambacho kinaweza kuonekana au kufahamika(common) kuwa kina mama(wanawake) wengi kuwa huwa wanaongezeka uzito(gain weight) pindi wanapo jifungua(kupata mtoto) kwa mara ya kwanza na kuendelea. Sina hakika sana ila nadhani wengi wao hawaipendi hali hii. Kutokana na hili baadhi yao wamekuwa wakijaribu kupunguza ulaji wa vyakula bila mafanikio. Wengine wamejaribu kufanya mazoezi(gym) lakini haikuwasaidia. Wapo waliojaribu kutumia dawa(tiba mbadala/hospitali) lakini hawakupata matokeo waliyoyatarajia. Mimi kama mtu ninayeishi miongoni mwao nimeshaona hali hii ya kuongezeka uzito inawanyima raha baadhi yao hivyo nika sema ngoja nilete jambo hili hapa jf ili wataalamu au wale waliopitia hali hii na kupata ufumbuzi, waje kutoa maoni na ushauri kwa mama zetu. Ningefurahi pia mtu akitoa ushauri azingatie kuwa anatoa kwa mtu anaye nyonyesha pia kwa yule ambaye amemuachisha mtoto kunyonya. Aidha kwa lengo la kujifunza, ningependa kufahamu nini hupeleka kina mama(siyo wote) kuongezeka uzito baada ya kujifunfua.
Asanteni na karibuni sana kwa mchango.
 
wengi huwa wanakula vyakula vinavyoweza kusababisha maziwa yatoke mengi, na vyakula hivyo pia huwaongeza mafuta mwilini na hivyo kuongezeka uzito
 
wengi huwa wanakula vyakula vinavyoweza kusababisha maziwa yatoke mengi, na vyakula hivyo pia huwaongeza mafuta mwilini na hivyo kuongezeka uzito

Asante sana kwa kutupatia sababu ambayo iko very logical.
Ila tunawasaidiaje sasa ili waendelee kupata maziwa ya kutosha lakini wasi-gain sana weight?
Halafu hilijambo mbona haliko common sana kwa wenzetu weupe(wazungu etc)?
 
Nadhani ni Nature tu hiyo huwezi kuizuia!
Kwasisi wafugaji hata mifugo ya kike ( ng'ombe, mbuzi, nguruwe etc)ikizaa inatanuka sana!

#NB
nimezungumza kama mwananchi mwenye uelewa wa chini sana juu ya hayo mambo!

Nimezingatia hiyo NB(nadhani nakumbuka mchango wako kwenye uzi fulani, some times back.)
Dose that mean we are helpless? Yaani hakuna namna kabisa kwa kuwa ni "nature"?
 
Yeah i can imagine, nimeona mke wangu anavyosumbuka, kimsingi hiyo inatokana na vyakula mama anavyokula kabla na baada ya kujifungua kwa manufaa ya kitoto kichanga. Hivyo ongezeko hilo ni la haki na kwa manufaa ya kichanga. Kuongezeka uzito si vibaya kwa mtu ambaye uzito wake haujafikia kiwango kinacho pendekezwa na wataalamu wa afya. Ofcause ni mbaya kwa yule ambaye ongezeko la uzito limeenda way beyond uzito pendekezwa. Nini kifanyike, kwakua huyo mama yuko kwenye kipindi muhimu cha malezi, anapaswa afuate maelekezo ya wataalam wa afya ili kujua nini ale nini aache kula bila ya kumdhuru mtoto
 

Hili jibu litatoa relief sana kwa mama zetu.
 
Umetumia mfano wa wamama wa kizungu hivi kweli nao wananyonyesha muda mwingi kama waafrika? Mimi nazungumzia uzoefu, mtoto wangu alizaliwa akawa na njaa ya hatari, ananyonya usiku kucha hadi unamhurumia mama yake, mama akitoka hapo ana njaa kali inabidi ale tu. Matokeo akawa kibonge [emoji23] ila baada ya kumaliza kunyonyesha ameweza kuubalance mwili japo si katika hali yake ya awali.

Hivyo nadhani chanzo ni Ulaji wa mtoto.
 
Ni vyakula tu, wengi wetu tunaamini sana katika kula kula mala kwa mala ili maziwa yatoke ila tunasahau kipi chakula bora kwa mama anyonyeshae.
Pili wale waliona uwezo ndio kipindi hiki hawafanyi kazi yoyote kisa mzazi, sasa kula mala kwa mala jumlisha hufanyi kazi...mwili unazidi kufutuka
ukienda vijijini hukuti mama aliejifungua kanenenpa, maana baada ya kujifungua anarudi home na kuendelea na jambe kama kawa, chakula ni mbogamboga ugali/ maharage na kama ni nyama mala moja moja na mwili una choma mafuta maana kazi zote anafanya mwenyewe.

mimi kwa uzoefu wangu ni kula matunda mboga mboga kunywa maji kwa sana na nyonyesha kila mala mtoto anapohitaji kunyonya
Kunyonyesha hupunguza mwili wa uzazi vizuri, ila wamama wengi siku hizi wanawapa watoto maziwa ya kopo, sijui kama ni sababu za ki afya ama u busy wa mama.
 

Sijakupata vizuri hapo kwenye bold.
Sjui kama hiyo inahusiana sana na kuongezeka uzito.
 

Mwenye masikio na asikie.
Asante mkuu.
 
Mwenye masikio na asikie.
Asante mkuu.
Watu tumeachana na natural food tupo busy na soseji, mala mavyakula ya lugeni kibao, yamekaa kwenye mikopooo weee ikifika bongo tunafakamia tu hahaha.
tembele maharage tumeshau
 
Watu tumeachana na natural food tupo busy na soseji, mala mavyakula ya lugeni kibao, yamekaa kwenye mikopooo weee ikifika bongo tunafakamia tu hahaha.
tembele maharage tumeshau
Asante.
 
Sijakupata vizuri hapo kwenye bold.
Sjui kama hiyo inahusiana sana na kuongezeka uzito.
Kwasababu mama anaenyonyesha vizuri hupata njaa zaidi na hula chakula zaidi.
 
Kwasababu mama anaenyonyesha vizuri hupata njaa zaidi na hula chakula zaidi.
Ikiwa hivyo njaa na uzito vinge-cancel one another na mama angebaki vile alivyo.
 
Samahani Carla, vp kwa ngozi nyeupe huko hujafanya kautafiti ukiondoa Rafiki zangu wa asili ya India. Wao wakoje baada ya kutuleta duniani sisi Bin/Bint Adam(s)
 
Kula mno baada ya kujifingua ni sababu kubwa na tamaa ya misosi ukiwa mjamzito.Haikwepeki mtanenepa tu.
 
Kweli kabisa njaa yake si ya nchi hii unawez kula ata ugali usiku wa manane ata sishangai yalishanikutaga
 
Samahani Carla, vp kwa ngozi nyeupe huko hujafanya kautafiti ukiondoa Rafiki zangu wa asili ya India. Wao wakoje baada ya kutuleta duniani sisi Bin/Bint Adam(s)

Kwa wenzetu weupe naona hali iko tofauti sana.
Ila pamoja na sababu nyingine, nadhani evolution, adaptation na geographical reasons zinachangia wao kuwa walivyo.(ni mtazamo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…