Ni kitu ambacho kinaweza kuonekana au kufahamika(common) kuwa kina mama(wanawake) wengi kuwa huwa wanaongezeka uzito(gain weight) pindi wanapo jifungua(kupata mtoto) kwa mara ya kwanza na kuendelea. Sina hakika sana ila nadhani wengi wao hawaipendi hali hii. Kutokana na hili baadhi yao wamekuwa wakijaribu kupunguza ulaji wa vyakula bila mafanikio. Wengine wamejaribu kufanya mazoezi(gym) lakini haikuwasaidia. Wapo waliojaribu kutumia dawa(tiba mbadala/hospitali) lakini hawakupata matokeo waliyoyatarajia. Mimi kama mtu ninayeishi miongoni mwao nimeshaona hali hii ya kuongezeka uzito inawanyima raha baadhi yao hivyo nika sema ngoja nilete jambo hili hapa jf ili wataalamu au wale waliopitia hali hii na kupata ufumbuzi, waje kutoa maoni na ushauri kwa mama zetu. Ningefurahi pia mtu akitoa ushauri azingatie kuwa anatoa kwa mtu anaye nyonyesha pia kwa yule ambaye amemuachisha mtoto kunyonya. Aidha kwa lengo la kujifunza, ningependa kufahamu nini hupeleka kina mama(siyo wote) kuongezeka uzito baada ya kujifunfua.
Asanteni na karibuni sana kwa mchango.
Asanteni na karibuni sana kwa mchango.