Naomba kuuliza ni biashara gani yenye kuanzia mtaji mdogo na faida yake ikaonekana mapema?

Uza matunda ya kukata kwenye take away.
Then wapitishie huko maofisin kwao kwa oda
 
Wazo lako ni nzuri na sikupingi, ila kwa ushauri wangu kama unataka kufanya kitu endelevu na cha manufaa ya mda mrefu... jifunze kuanza kwa kupata hamna kwanza halafu ndio uanze kukokotoa hesabu ya hamna hadi faida ya asilimia hamsin hadi Sabini shida kubwa watu wengi tunataka kufanya kitu chenye kuanza na faida hapo hapo. Au uanzishe kitu cha kuuzika nusu mzigo siku ya kwanza au kufungua duka la kujaza wateja siku ya kwanza.... ukweli ni huu, hata kama bidhaa inauzika vipi na inatoka kwa speed kubwa kwa watu wengine. Ni ngumu sana kwako kutoka hivyo kwa siku ya kwanza kwako wewe ambaye ni mgeni kuuza. Hivyo jifunze kuwa mvumilivu.
Mfano wangu ni kuwa. Mimi nilianza kwa kuuza karanga kilo tano kwa miezi mitatu, na ilifikia hatua hadi inabidi mwenye duka aanze kuzitumia mwenyewe... na ilifikia mahali hadi sehem wanachukua mzigo lakini nikipita baada ya miezi miwili nakuta mzigo haujatoka Yaani naondoka bila kuaga. Lakini leo mwezi wa kumi nauza kilo hamsini kwa wiki Yaani oda zinanizidi lakini haikuwa rahisi
 
Biko vipi? (Jokes)

Bora ungesema huo mtaji wako mdogo ni sh ngapi maana tunatofautiana mitazamo unaweza wewe kuona mtaji mdogo kumbe sisi tunaona mkubwa au kinyume
 
Kwa wachangiaji wote me naona wako sahihi katika mawazo yao kitu cha kuongezea hapo ni kwamba jambo la kwanza jiamini ktk mtaji ulio nao na utambue kuwa nikama mkulima aliye shika mbegu mkononi akiwa shamban tayari kwa kuzipanda hivyo huwa na matumaini kuwa zitaota.
Jambo la 2. Unapotaka anzisha biashara yoyote angalia location hii ni sawa na unapopanda mbengu usije ukaitupa kwenye mwamba ikashindwa kuota.
3. Usisikie maneno ya watu wenye kkkatisha tamaa.
Jiamini ktk biasha unayofanya.
Mwisho biashaya inayoanza na mtaji mdogo ni samaki, mboga mboga, matunda n.k
 
Mkuu hizo karanga unauzaje, fafanua kidogo, na Wateja wako ni watu gani?
 
Reactions: lup
Ungekua wa kike ningekushauri utengeneze mafuta ya urembo ya wanawake
 
Umeongea bonge la point aisee bg up
 
Hivi inawezekana vipi mtu kuomba ushauri wa biashara wakati wewe hauna hata wazo la nini unadhani unaweza ukafanya...[emoji52] [emoji52] .
Binafsi nimekua naamini kwamba unapaswa kuanza na wazo, then pesa, kisha ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…