Naomba maana ya neno COMPROMISE katika Kiswahili

Naomba maana ya neno COMPROMISE katika Kiswahili

Compromize maana yake ni mapatano au makubaliano hasa ya kifedha, mfano unaponunua nguo
 
makubaliano ya kibiashara,mfano umeenda dukani kununua kiatu muuzaji akakuambia tsh 100000/-wewe ukamwambia nakupa 75000/-mkavutanavutana akakuambia bas lete 85000/-we nae ukabana ukamwambia nakupa 80000/-muuzaji akakuambia basi lete 83000/-na ww ukamwambia nakupa 82000/-nibaki na buku la nauli,muuzaji akakubali hiyo inaitwa compromise yaani we are argued for a long time but finally arrived at a compromise
 
"Lakini usomaji wangu wa awali unaniambia kwamba Rasimu hii ni maelewano kwa maana ya compromise, na sio mapatano, au mwafaka, kwa maana ya consensus. Nijieleze kidogo. Katika maelewano au compromise, pande zinazokinzana hatimaye zinakubali kwa shingo upande ili kutokwamisha maamuzi. Pande zote zinapata kidogo na kupoteza kidogo, na kila upande huwa na mkakati wake wa kupata zaidi katika duru ya pili. Kwa hivyo, maelewano kamwe hayawezi kuwa kwa moyo safi. Maelewano au compromise, yanazaa uamuzi legelege. Mapatano au consensus, kwa upande mwingine, ni maafikiano yanayofikiwa baada ya mjadala mrefu, kila mmoja akilenga kuthibitisha hoja yake na kwa njia hii kusadikisha wenzake kwamba hoja yake ni sahihi. Baada ya kufikia uamuzi wa mwafaka, kila mmoja anatoka akiwa ameridhika na amefurahi. Katika compromise, kila mmoja anatoka amenuna. Ni wazi kwamba huwezi ukapata mwafaka fastafasta. Lazima utachukua muda" - Issa Shivji (2013), Ukurasa wa 7-8, Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu ya Katiba Mpya: Mhadhara wa Kuaga Kigoda cha [Taaluma cha] Mwalimu [Nyerere Chuo Kikuu cha Dar es Salaam]
 
makubaliano ya kibiashara,mfano umeenda dukani kununua kiatu muuzaji akakuambia tsh 100000/-wewe ukamwambia nakupa 75000/-mkavutanavutana akakuambia bas lete 85000/-we nae ukabana ukamwambia nakupa 80000/-muuzaji akakuambia basi lete 83000/-na ww ukamwambia nakupa 82000/-nibaki na buku la nauli,muuzaji akakubali hiyo inaitwa compromise yaani we are argued for a long time but finally arrived at a compromise

ahsante mkuu nimeelewa
 
Back
Top Bottom