Naomba Majibu Tafadhali: 'Mfumo imara' ni nini?

Unapoambiwa mifumo imara maana yake ni kwamba nchi inakua ya wananchi na wote kuanzia rais na taasisi nyingine zote za serikali watawajibika kwa wananchi kupitia taratibu zilizowekwa na kama kuna kasoro au mianya yoyote yakuenenda tofauti na miongozo hatua zinachukulika automatic.
 
Taifa halijawahi na haliwezi kupata hasara kwa kumpoteza kiongozi wa aina yoyote mkuu,
no one is indispensable under the sun.(JFK)
Na ndiyo maana Mama anasema "Kazi iendelee.
Nakubali kama taifa we are stronger, na katikati yetu tuna hazina ya watu bora na wanaotufaa/watakaotufaa sana kama taifa kwa nafasi zao, uwezo wao na potential zao.

Lakini hilo halimaanishi kwamba you can just do away with anybody however you like eti kisa no one is dispensable. Hiyo ni model mbaya sana, na ndio maana nchi huwa zina vipindi vya prosperity na vipindi vya depression. Tanzania iliyoongozwa na Nyerere ni tofauti na Tanzania iliyoongozwa na Mwinyi ni tofauti na Tanzania iliyoongozwa Mkapa ni tofauti na Tanzania iliyoongozwa na JK ni tofauti na Tanzania iliyoongozwa na JPM. Kama katiba ni ile ile kwa nini ladha za uongozi ziwe tofauti? Kuignore impact ya mtu ni willfull ignorance, na ni hatari sana, maana inajenga tabia kwamba mtu yeyote anaweza kuwa eti kwa vile kuna katiba na job descriptions.
 
Nyerere ndiye aliyewaloga Watanzania waone kuwa ni bora watawaliwe kidikteta badala ya kufata mfumo wa kidemokrasia. Lazima ukubali Nyerere alikuwa ni genius. Na Watanzania walikubali. Wachache waliompinga walipotezwa au walikimbia nchi. Kwa hiyo kutawaliwa kidikteta ndiyo msingi wa nchi hii aliotuachia baba wa taifa na mpaka leo upo. Mfumo imara unapingwa kwa sababu msingi uliojengewa nchi hii ni kutawaliwa kidikteta.
 
Sidhani kama inawezekana mtu kuwa na control kwa kila kitu katika uongozi wa taasisi yoyote hata ngazi ya familia, achilia mbali ngazi ya taifa. Tunaposema mtu ni nguzo hatumaanishi mtu awe omnipotent, omniscient na omnipresent. Mtu hawezi kuwa hivyo, mtu si Mungu.

Ila tunachomaanisha ni kwamba mtu anapaswa kufanya intervention katika mifumo ya binadamu pale inapobidi. Watu wana talanta zao, wana maarifa yao, wana utashi wao, na wana gut insticts zao. Kuzizuia zisifanye kazi eti aache mfumo ufanye kazi ni kuzuia ubunifu, ni kuzuia potential za mtu zisifanye kazi.

Mama Samia kuagiza BOT ifanyiwe special audits inadhihirisha jinsi usivyoweza kuachia tu mifumo ijifanyie mambo yao yaliyopo kikanuni. Kwa nini ameagiza BOT ifanyiwe special audit? Hatuwezi kujua kwa uhakika, lakini kwangu mimi it is OK, namtegemea mama asikalie kile kiti kama robot. Kama kuna taarifa kazipata, kama ana gut insticts kwamba kuna mambo hayaendi ndivyo sivyo, kama kuna namna nyingine iliyomtuma afanye hivyo, wacha afanye. Anautendea haki ubinadamu wake, anaitendea haki nafasi yake, kama mtu binafsi.
 
Si ndivyo mfumo wetu ulivyo? Kipi kimebadilika? Katiba yetu inamtaja Rais anachaguliwa na wananchi na anawajibika kwa wananchi. Kama akienda ndivyo sivyo wananchi kupitia bunge letu linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, na bunge likavunjwa na kurudi kwenye uchaguzi.

Huo sio mfumo? Una shida yoyote?
 
Mkuu, ukichunguza uzi huu utagundua ninafuatilia kila bandiko linalowekwa hapa. Lengo, nipate majibu nijifunze. Mwisho wa siku kwa pamoja tuamue kipi kinatufaa kama taifa, kwa msingi ule ule wa kuendeleza umoja, amani, ushirikiano,na ustawi katika nyanja zote za nchi yetu Tanzania. Binafsi nina imani na nguvu ya JF kufikisha ujumbe panapohusika.

Kwa msingi huo, bandiko lako limenichanganya hasa ukizingatia swali la msingi la uzi huu. 'Mfumo imara' ni nini?

Kwa hiyo, Mkuu naomba udadavue tena hoja yako. Natanguliza shukrani.
 
Naweza kupendekeza hivi: kwamba tupalilie watu bora watakaotengeneza mifumo bora itakayosimamiwa na watu bora. "Standing on the shoulders of giants" wao wanasema. Inapotokea mtu imara na akaonyesha umahiri huyo ni asset , na hata akifa, kama tulivyompoteza JPM, we build on his legacy. Mfumo imara kuliko yote kwangu mimi si sheria na wala si katiba. Mfumo imara ninavyouona mimi ni mila, desturi na utamaduni. Vitu, dhana, legacies na practices zikiwa codified hadi zikawa sehemu ya mila, desturi na utamaduni wa watu fulani au taifa fulani ni vigumu sana kuvifuta. Kama kuna kitu ni kizuri na tunadhani ni vizuri tukijengee mfumo imara ili isiwe rahisi kupotea, basi kitafutuwe namna kiwe sehemu ya mila, desturi na utamaduni wetu. Na kuna njia kadha wa kadha za kufanya hivyo.
 
Hovyoo...!!

Jiwe hajawahi kua na mfumo imala.
Badala yake.alikua anafanya mambo anavyota.

Nakumbuka zama za kizazi kile kabla ya watu hasa watanzania kwenye sehemu zao za kazi akiingua meneja au mkurugenzi watu wanatetemeka.

Tofauti na sasa watu wanasomea uongozi wanajua haki na wajibu wa kila mmoja ktk sehemu yake ya kazi kwenye ofice yake.

H.R.
Atampa mkataba mfanyakazi kuanzia muda wa kuingia kazini ,muda wa kula,muda wa kufunga kazi na hata mavazi.
Na ili mtu asizalilishwe kwenye ofisi yake kwa kufokewa kama alivyokua anafanya jiwe kwa wasaidizi wake sheria(mfumo imara wa H.R) Unambana mfanyakazi hadi mkuruenzi ndani ya ofisi.
Hapa tunaona sasa mfumo imala unambana kuanzia mfanyakaz wa chini kabisa hadi mkurugenzi mwenye idara,ofisi,au kampuni hasa kwa mfano muda wa kufika kazini au mavazi bila ya ugomvi au kofokeana.

Kiongozi na mfanyakazi wanacheka na wanafulahi pamoja lakini mwisho wa siku mmoja wapo atabanwa na mfumo imara ana anaweza kutolewa au kutoka kazi kutokana na sheria (mfumo uliowekwa.

Mfano:-
Mkataba ,sheria(mfumo )unakwambia uingie kazini saa 2 kamili asubuhi utakuta daftari la kusini muda ulifika.
Ikifika saa saa2 na robo HR anachukua daftari anapiga mstar mwisho wa.kolamu ya wafanyakazi.wanaoingia hivyo wewe uliochelewa utakua nje ya mstari,HR haongei na wewe.

Mwisho wa mwezi tunakaa kikao cha.mwez tunakuona wewe ulikua nje ya msatar kalibu mala 10.
Maana yake mchelewaji sugu kazini.
HR anakuandikisha maelezo ya uchelewaji kama onyo.
Ukirudia mala 2 au 3 utakua umejifukuzisha

Ndio hivyohivyo kwa mkurugenzi nae akilewa madaraka kila siku anafika ofisini sa 4 na menejiment inasubili mafaili yalioko mezani.yasainiwe ili kazi ziende yeye hayupo maanayake nayeye anahatari ya kujihalibia hazi au kutaka kujifiris.

Hivyo MFUMO IMARA NI KATIBA IMARA INAYOWEZA KUMBANA KILA MMOJA KUANZIA MFANYAKAZI WA CHINI KABISA HADI MKURUGENZI, BIRA YA KUSUKUMANA.

Nakumbuka jk nyerere aliwahi kusema kwenye hotuba zake kua.
Katiba hii ya sasa akitokea mtu mwenye roho mbaya atawaburuza sana wananchi.

Hivi tujiulize hii leo Rais akisema hela zote zilizokuwemo benk kuu ni zangu na hata akizichukua hakuna wa kumshitaki.

Huu ni ujinanga na upuzi wa hali yajuu kabisa.

Ndio maana jiwe alijua amelewa madalaka hadi ananunua kuku au muhindi wa.kuchoma kwa elf50 hadi laki.
Na kugawa au kutumia hela vile anavyoona inafaa yeye kama yeye.
 
Kwa kifupi sana
Mfumo imara ni pale ambapo nchj inakuwa na katiba imara inayozipa nguvu na uhuru taasisi zake kutekeleza majukumu ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi bila kuingiliwa kwa namna yoyote ile.Ili serikali iweze kuwajibika ipasavyo kwa wanachi walioiweka madarakani.(Social accountability and right based approach).
Taasisi hizo ni pamoja na;
1.tume huru ya uchaguzi
2.Bunge
3.Mahakama
4.CAG
5.Baraza la madiwani.
Maana yake ni kwamba taasisi hizi zikiwa imara na zikatekeleza majukumu yake bila kuingiliwa,Serikali itawajibika vilivyo kwa wananchi walioiweka madarakani,kwa kuogopa kuondolewa madarakani na hata kushitakiwa na kufungwa bila kujali nafasi aliyonayo kiongozi yeyote awae, pale watakapo shindwa kutimiza wajibu wao au kufanya ubadhilifu wa Mali ya umma au kutoa maamuzi yanayoweza kuisabishia nchi hasara ya Mali na watu.
Misingi imara ya kitaasisi inapelekea kuwa na Serikali inayowajibika kwa umma badala ya umma kuwajibika kwa serikali.
 
Mama Samia kuagiza BOT ifanyiwe special audits inadhihirisha jinsi usivyoweza kuachia tu mifumo ijifanyie mambo yao yaliyopo kikanuni
Maana yake mfumo umefeli, imagine kama rais mwenyewe angekuwa anahusika. Maana yake asingetoa hiyo order, na hakuna kile kingefanyika.

Kunatakiwa kuwe na layers nyingi zinazotazama uwajibikaji. US wana office za Inspector General kwenye key institutions. Kazi yake ni kudeal na misconducts za taasisi, mfanyakazi wa taasisi akiona issue ya hovyo inataka au inafanyika, na kama yeye hawezi kuzuia, anareport kwa IG. Na IG anatakiwa achunguze na analazimika kupeleka taarifa kwenye kamati ya sekta yake bungeni kuhusu malalamiko ya mfanyakazi. Akishindwa, mfanyakazi anaruhusiwa kuifuata kamati ya bungeni kuhusu IG kutofikisha report yake.

Kamati zao za bunge zina viongozi wa chama tawala na upinzani. Kukiwa na uchafu, sio kila mtu anavumilia, swali ni je kuna mfumo wa mtu mdogo kama junior accountant kwenye wizara au taasisi kujaribu kirekebisha? Wenzetu hapa wamekwenda mbali na kulihusisha hata bunge, maana vitu vingine serikali itaminya kwa sababu ni aibu yao. Accountability haitakiwi kuwa hisani ya kiongozi mmoja, jana Kakoko anaonekana wa maana, leo anaonekana hafai, nani anajua kesho itakuwaje.
 
Umejaribu kuwaza kuhusu hizo cost implications za hizo layers za uwajibikaji? Tayari Tanzania ina changamoto ya kuwa na serikali kubwa, na kubuni layers za checks and balances za ziada ndani ya serikali isije ikawa ni kuiongezea uzito wa kibudget serikali, na hilo maana yake ni kutengeneza serikali yenye matumizi oversize.

Tanzania tuna tabia ya kusolve tatizo moja kwa kutengeneza tatizo jingine. Kama kuna tatizo la rushwa, basi unda taasisi uiite PCCB, PCCB ikienda kumkamata mla rushwa au mpokea rushwa, rushwa zaidi inafanyika hili mtuhumiwa asikamatwe. Perpertual cycle of corruption!

Kumodel kile wanachokifanya Marekani hapa Tanzania haiwezi kuwa bila na changamoto zake. Changamoto ya kwanza ninayoiona ni kwamba Marekani wanaishi kwenye social-economic climate tofauti na Tanzania. Kule private-sector ina nguvu na inainfluence kile kinachofanyika serikalini. Checks and balances, na levels za uwajibikaji zinazooperate kwenye private corporations kama microsoft zimekuwa modeled hata ndani ya public institutions za Marekani. Bosi wako immediate asiporidhika na utendaji anakufire tu, na ile inaleta discipline ya hali ya juu. Ila kwa nchi yetu iliyojengwa kwenye misingi ya kijamaa, ukiintroduce hiyo model utayasikia hayo mayowe. JPM si ndicho alichokuwa akifanya? Kwake aliichukulia Tanzania kama kampuni na yeye akiwa kama CEO, alitaka matokeo, tena matokeo sasa. Alipoanza kutumbua tumbua (private sector huwafire waajiriwa namna hii hii) nadhani uliyasikia mayowe. In short JPM alioperate bila kujijua kama maCEO wa big corporations wanavyooperate.
 
Nina wasiwasi hapa kuna watu wanajadili lakini hata maana ya neno lenyewe mfumo hawaijui.

Mfumo kwa kiingereza ni system, ikiwa na maana ni mchanganyiko wa vitu vinavyofanya kazi kwa pamoja ili kukikamilisha, mfano mfumo wa lugha unaunganisha vitu kama sauti, silabi, sentensi na tungo, au music system inaunganisha vitu kadhaa ili kuunda kimoja kinachoeleweka ndio maana tunaenda dukani kununua subwoofer.

Mpak kufikia hapa utaona wale wanaoamini mfumo unaundwa na individual person wanakosea, hakuna mfumo unaoundwa na mtu au kitu kimoja, lazima viungane vitu kadhaa ili kufanya kimoja kilicho kamili, hiyo ndio maana ya mfumo.
 
Kuhusu cost, kila kitu kina gharama. Ingawa kuna vingine tayari vipo kama kamati za bunge. Shida ni kuzitoa meno. Hata kufanya kazi zake zinashindwa
 
Wewe ulipenda 'Mtu imara', yupo wapi sasa..analiwa na mafunza huko. Utakaa unamlilia mpaka lini?
 
Hakuna mfumo wa namna nyingine utakaowezekana kwa nchi hii. Nchi hii msingi wake ulichimbwa na Nyerere ili tuongozwe kidikteta. Na huo ndiyo mfumo mpaka leo tunaufata na ni imara hapa. Na ukijaribu kuubadilisha mfumo tulionao, nchi itasambaratika halafu tutaanza upya tena. Ndiyo maana nchi nyingi zinazoongozwa kiditekta zikibadilisha mfumo zinasambaratika. Mfano mzuri ni nchi kama Iraq baada ya Wamarekani kumtoa Saddam na kuwaletea demokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…