Naomba makadirio ya Mabati

nyamalagala

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2016
Posts
744
Reaction score
673
Habari ndugu zangu. Leo nimekuja kwenu kuomba wajuzi wa mambo ya ujenzi.
Nina boma langu limenisotesha kulimaliza mpaka kozi 12.

Sasa hatua inayofuata ni kupaua. Hitaji langu ni kujua idadi ya bati zitakazotumika. Boma langu lina sifa zifuatazo:

1. Urefu futi 37

2. Upana futi 22.10

3. Vyumba vitatu (kimoja ni master vingine ni vya kawaida).

4. Kuna public toilet, jiko, stoo na dinning.

Karibuni sana kwa mwongozo.
 
(((37 x 30.45) + (40 x 2)) / 70) x 4 = 68 pcs

Andaa Bati 68 za futi 10, Kama utatumia bati za kupima, nunua bati 34pc za futi 18

Mnaohitaji kufanyiwa makadirio ya ujenzi, tuwasilianeni

Assumption
  • Upana wa bati 80cm+
  • Urefu wa bati 300cm or 3m
  • Overhang 40cm pande zote
  • Mgongo wa tembo (mchoro wa paa haupo)
 
Shukran sana mkuu. Sasa nimepata pa kuanzia. Ubarikiwe mno
 
Mkuu we ni muhimu sana jukwaani, kwasababu umempa mwongozo mzuri
 
Natamani kujua ufafanuzi wa hii hesabu ndugu[emoji120]
 
Hizo ni taaluma za watu, hata hiyo 4 unayoiona hapo ina formula yake jinsi ya kuipata...hapo nimerahisisha tu ili mambo yasiwe mengi. Lazima uwe na basics navyo, vinginevyo utakuwa unakariri
Sawa mkuu fanya tu kunipa darasa kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…