Naomba mbinu ili niweze kufahamu kingereza kwa ufasaha

kajugu

Senior Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
122
Reaction score
20
Wadau naomba mnisaidie mbinu mbalimbali ili niweze kujua kingereza kwa ufasaha..
 
Mi natumia njia rahisi sana, nashinda sana kuangalia muvie na kusoma vitabu.

Ila kabla hujaanza kuitumia hii njia, jifunze simple grammar.
 
Kunywa pombe yai litapanda tu

Mkuu Bufa kuna jamaa leo nimemkuta kishalewa bado kidogo anitoe knok out kwa ngeri,lakini na mimi nilipopata laga tatu jamaa kanikimbia.
 
Last edited by a moderator:

Bora umeleta ushuhuda mkuu tena wa wewe mwenyewe sio hata wa kusimuliwa. Jamaa nadhani kashapata dawa ya ugonjwa wa kimombo, lager tatu au zaidi kama ulimi wake mzito sana kusema YES na NO.

Kula bia yai litapanda tu.
 
Last edited by a moderator:
andikeni tense wadahu kwenye post hii mwanzo mwisho.present tens,past tense na future tense.FANYENI HIVYO WADAU ITAKUWA SAFI SAAAANAAA.KWA WALE AMBAO HATUJUHI.
 
Kwanza kabisa uwe na nia na usione aibu kuongea mbele ya watu. Jihusishe na watu kama wewe wanaotaka kukifahamu vizuri au kuwa na marafiki kisha mnakuwa mnajenga mazoea ya kuongea kwa kizungu, kuanzia stori za kawaida mpaka kila kitu. Pia kuwa na mazoea ya kuangalia movies za kizungu (sio za kinaigeria) na pia angalia news za kizungu bbc, skynews, algezira, supersports na pia redio za kizungu. Yaani ukisikia chaneli ya kizungu wee ganda hapo, hakikisha unapenda vitabu vya grammer pia. Mimi siko fit pia ila nimetumia hizi mbinu na kuna mabadiliko makubwa sana. Siku hizi cnn, bbc hata watiririke kiasi gani hawaniachi. Documentaries hawaniachi. Kuongea napo nina mabadiliko makubwa. Huwezi amini, kwa mbinu hii naanza hata kujua kifaransa. Nasikiliza sana RFI ktk Azam Tv upande wa redio. Cha msingi ni kukuambia kuwa hizo mbinu hapo juu zafanya kazi endapo utazizingatia kujifunza lugha yeyote. USIONE AIBU, watakaokucheka, waache wacheke, wabongo wengi hawajui lughqa na ukianza kuongea, wanakaa stand by ukosee waanze kukukosoa, ila wao cha kushangaza hawazungumzi. Kazqa buti.
 
Huu ushauri wako unatosha sana mkuu. Hizi njia nimezitumia sana. Nyingine nilikuwa napenda kununua magazeti yenye nyimbo. Pia nilibahatika kufanya kazi katika kampuni moja hivi ilikuwa na wafanyakazi kutoka Uganda, Marekani, Kenya, Ufilipino, Uingereza, Indonesia, Srilanka na Scotland kwa miaka miwili na media hapo ni English. Kwakweli ilinijenga sana na kunipa ujasiri bila kuwaza mbele ya watu.
 
Back
Top Bottom