Kwanza kabisa uwe na nia na usione aibu kuongea mbele ya watu. Jihusishe na watu kama wewe wanaotaka kukifahamu vizuri au kuwa na marafiki kisha mnakuwa mnajenga mazoea ya kuongea kwa kizungu, kuanzia stori za kawaida mpaka kila kitu. Pia kuwa na mazoea ya kuangalia movies za kizungu (sio za kinaigeria) na pia angalia news za kizungu bbc, skynews, algezira, supersports na pia redio za kizungu. Yaani ukisikia chaneli ya kizungu wee ganda hapo, hakikisha unapenda vitabu vya grammer pia. Mimi siko fit pia ila nimetumia hizi mbinu na kuna mabadiliko makubwa sana. Siku hizi cnn, bbc hata watiririke kiasi gani hawaniachi. Documentaries hawaniachi. Kuongea napo nina mabadiliko makubwa. Huwezi amini, kwa mbinu hii naanza hata kujua kifaransa. Nasikiliza sana RFI ktk Azam Tv upande wa redio. Cha msingi ni kukuambia kuwa hizo mbinu hapo juu zafanya kazi endapo utazizingatia kujifunza lugha yeyote. USIONE AIBU, watakaokucheka, waache wacheke, wabongo wengi hawajui lughqa na ukianza kuongea, wanakaa stand by ukosee waanze kukukosoa, ila wao cha kushangaza hawazungumzi. Kazqa buti.