Naomba mbinu ya kuzuia vicheche bandani

Naomba mbinu ya kuzuia vicheche bandani

Mama Nehemiah

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2018
Posts
244
Reaction score
439
Wakuu naomba maarifa ya jinsi ya kuwazuia vicheche maana wanaingia bandani kwa kuku wanakula mayai.
Mahali ninapoishi kuna uzio wa senyeng'e so wanaingia mahali kuku hutaga na kuchukua mayai.

Mbwa kwa sasa siwezi kufuga naombeni njia njingine tafadhali.
 
Saga pilipili kisha pulizia kunguka banda.

IMG-20221129-WA0000.jpg
Screenshot_20221129_082441.jpg
Screenshot_20221129_082432.jpg
Screenshot_20221129_082456.jpg
Screenshot_20221129_082527.jpg
 
Kicheche huwa wanakula kuku piya, chunguza vizuri kinachokula mayai, inawezekana panya ndiyo wanaokula mayai.

Kicheche kikiingia katika banda la kuku huwa wanakamata kuku siyo mayai.
 
Kicheche huwa wanakula kuku piya, chunguza vizuri kinachokula mayai, inawezekana panya ndiyo wanaokula mayai.

Kicheche kikiingia katika banda la kuku huwa wanakamata kuku siyo mayai.
Nimeshawashuhudia kwa macho yangu ni vicheche,yes wanakula kuku pia walishanilia kuku wadogo..wanawakata shingo wanakunywa damu unakuta mzoga tu.
 
Hahaha nimejaribu kufikiria kama ndo raia unapewa yai viza lililochemshwa, nimecheka sana[emoji23].
Imagine anakula kicheche halafu likifika tumboni digestion inashindwa kufanyika [emoji23] atatamani kurudi kinyumenyume bandani alinye kama lilivyo maana kulitapika hawezi
 
Wategee mayai viza yaliyochemshwa
Mkuu kicheche hamezi yai kama kenge, kama halijapasuka hali. Kicheche akija kula mayai bandani utajua kwa sbb utakuta mayai yamevunjwa sana. Huwa wanayapigiza mayai kwenye ukuta yakivunjika wanakula. Kwa maana hiyo yai la kuchemsha halimtegi kicheche
 
Back
Top Bottom