Naomba mbinu za kumdai mdeni wangu sugu

Naomba mbinu za kumdai mdeni wangu sugu

Sic March

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2019
Posts
690
Reaction score
906
Habari wanaJF, heri ya mwaka mpya japo mwaka unaenda kasi sana huwezi amini leo ni weekend dah, tuachane na hayo.

Naombeni msaada maana huyu mdai wangu kawa sugu na misemo ya kila aina.

Hebu fikria unadai mtu anakwambia kauli kama hii "Najua unanidai lakini usinidai hivyo mimi nikipata nitakupa maana hata mimi matatzo yangu sijayasajili BASATA au COSOTA kwamba ni yangu tu pekee".

Hivi ni mimi pekee ndio nakumbana na kasumba za kudai au mpaka nyie wenzangu na hizi kauli huko kwenu vipi mnapewa zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdeni wako utakuwa na uhakika hataki kukulipa kama unauhakika wa mapato yake labda ameajiriwa analipwa mshahara au anakijiwe cha biashara ukikitembelea unaona miamala ikipita. Zaidi ya hapo akikuambia hana vuta subira inabidi umuelewe. Ukimbananisha atakutolea povu sasa hafanyeje? Ulimkopesha kwa uaminifu ikiwa na maana ulimwamini na endelea kumwamini akisema hajapata kuwa mpole! Kuna watu wengine kama anakudai inakuwa kero. Mimi mwenyewe nadai watu kibao pia na mimi nadaiwa! Nashukuru Mungu wadeni wangu wananielewa na Mimi ninaowadai tunaendana mdogomdogo!
 
Kama una ushahidi wa watu Au maandishi mpeleke serikali za mitaa huko mfikie muafaka maana kwa majibu hayo mwisho wa siku msije mkagawanA majengo
Kesi za madai zote sikuhizi zinasikilizwa kata na s/mtaa
Polisi ni kuanzia madai ya mil3


Inaumiza sana pale mdeni wako unapomuona anatoboa tu alafu wewe anakujibu shombo bora mtu awe na kauli nzuri hata kama hana nia ya kulipa
 
Kama una ushahidi wa watu Au maandishi mpeleke serikali za mitaa huko mfikie muafaka maana kwa majibu hayo mwisho wa siku msije mkagawanA majengo
Kesi za madai zote sikuhizi zinasikilizwa kata na s/mtaa
Polisi ni kuanzia madai ya mil3


Inaumiza sana pale mdeni wako unapomuona anatoboa tu alafu wewe anakujibu shombo bora mtu awe na kauli nzuri hata kama hana nia ya kulipa
Kuna muda nikimuangalia nacheka mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anakuona zoba ndo mana anakujibu anavyoweza

Kuwa mpole,akijisikia atakulipa
 
Fanya mkutane siku moja ulizia pesa yako akisema hana mkiagana zoa nyayo zake hakikisha ameona ulichofanya lazima atakurudia na maswali mengi mfululizo mfululizo kama we unafanya nini, unataka kunifanya nini, hicho nini unazoa nk. We kaa kimya utashangaa anaanza kukuomba huo mchanga uliouzoa then hapo na we unasimika, mwambie nipe hela yangu nikurudishie nyayo zako. Waafeica wengi tunaamini katika Mungu mmoja ila ni waoga sana wa ushirikina. Hela utapata ndani ya muda mfupi
 
Back
Top Bottom