Naomba mnieleweshe maana ya ''ngekewa''

Naomba mnieleweshe maana ya ''ngekewa''

wakulichomeka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
517
Reaction score
142
Kuna kitu kinaitwa Ngekewa, kila mara nasikia eti fulani ana Ngekewa. Nimejiuliza maswali mengi sana sipati jibu, Ngekewa ni nini? Hebu nisaidieni Ngekewa ni nini?
 
Kunakitu kinaitwa ngekewa kilamara nackia eti furani anangekewa nimejiuliza maswali mengi sana spati jibu ngekewa nini hebu nisaidieni ngekewa ninini!!?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ngekewa
Ndere
Kismati
Nyota ya jaha
Karma nzuri
n.k.

Haya maneno yote yana maana ya kuwa na "bahati nzuri".

Ukiwa na ngekewa basi hata kama una bosi mkali namna gani, na hasa kama amekasirika, akikuona tu analainika kama siagi na kukupendelea wewe.

Pia kama kuna kabinti ambacho watu wanakaogopa kwa ukali wake, kama una ngekewa basi mijamaa yote itatemwa lakini ukitokea wewe tu mambo yanakuwa laini sana - just kidding.

Nasikia **** Sangoma wana mavumba ya kutoa hii ngekewa. Mkuu MziziMkavu njoo utusaidie. (habari za siku nyingi MziziMkavu).
 
Last edited by a moderator:
Kunakitu kinaitwa ngekewa kilamara nackia eti furani anangekewa nimejiuliza maswali mengi sana spati jibu ngekewa nini hebu nisaidieni ngekewa ninini!!?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Ngekewa
Ndere
Kismati
Nyota ya jaha
Karama nzuri
n.k.

Hayo maneno yote yana maana ya kuwa mtu na
"bahati nzuri".
 
Wakuu habari

Ngekewa ni nini, na kwa lugha ya Kingereza inaitwaje.

Msaada wa kuelewa Ngekewa.
 
Ngekewa ni bahati na kwa kiingereza inaitwa lucky.
Na mimi siyo mtaalamu wa kiswahili na pia kiingereza. Sijui kama ngekewa ni neno fasaha la kiswahili lakini kwa jinsi ambavyo limekuwa likitumika umaanisha bahati. Kwa kiingereza ni "luck" (badala ya lucky, kwa sababu lucky ni adjective). Pia maneno kama "chance" na "fortune" yanaweza kutumika. Pia kuna neno "kismat" linaweza kutumika japo naona pengine lina asili ya uarabuni na katika kiingereza utumika kwa mara chache. Sasa kuhusu kazi ya ngekewa hapo naona sina jibu la uhakika japo kwa haraka haraka naweza kusema kwamba kazi yake ni kuleta neema kwa aliyepata hiyo ngekewa.
 
nahisi ungepeleka jukwaa la lugha kule...ungepata msaada wa wataalam zaidi
 
No kunamnyama anaitwa ngekewa ndio maana cikupeleka kwenye jukwaa la lugha. Asanteni kwa maelezo lakini
 
Ngekewa: kule kwetu tunawaita Kidungu maria. Ni mnyama fulani mwenye muonekano wa Panya kwa sura ila umbile ni kama Nungu nungu anavimiba. Kuhusu kazi yake yeye ni kula tu ndio kilichomleta Duniani labda useme kazi yako wewe Binadamu kwake ni ipi? Kwa kiiengereza sijui wanaitwaje maana sijawahi kufika kule, kwanza sidhani kama wapo kule.
 
Ha! Ha! Kidungu maria duh!
 
Ngekewa, ukitaka kujua jinsi inavyofanya kaz, Nenda lindi wilaya ya liwale ulizia shm moja inaitwa "NGENDE" then uje ulete mrejesho usituumize kichwa hapa, Magu kashayavuruga haya maisha kbs unywaj wa bia umekuwa adim xna.
 
Unaongelea Hedgehog???
1455810107045.jpg
 
Swali lilikuwa tata. Kumbe ulimaanisha kile kimnyama kama nungunungu mdogo. Kule Mwanza kimezoeleka kwa jina la kalunguyeye. Kama ni huyu basi kwa kiingereza ni hedgehog.
 
Back
Top Bottom