Naomba mnifundishe kuendesha gari aina ya IST

Kuendesha gari rahisi sana ishu kubalance brake na speed ndo kazi ila utazoea cha kwanza endesha ukiwa PEKU 😀 😀 😀 Maana unaweza jikuta mtaroni mimi dalali alinipeleka mpaka kwenye uwanja mkubwa karibu na home mpaka kufika jioni nishajua mbona ushamba kurudi home nimepark funguo haitoki nachomoa wapii nkampigia dalali akawa hanielewi yani ila nikajiongeza nigoogle kumbe ufalaa gear bado ipo kwenye D
 
Kwa maelezo haya sitakwenda Driving school, ni kuingia tu barabarani na kupambana na watumiaji wengine😁.
 
Nipe darasa mzee maana baiskeli naweza ila pikipiki Sina ujanja nayo
Hakuna tofauti na gari, Tuanze na gari lenye manual gear yaani unabadili gia kwa kutumia vitu viwili mguu na mkono, mguu una kanyanga Klachi kwa mguu huku unabadilisha gia kwa utaratibu ufuatao
1. Hakikisha hand breki iko mahali pake imekaza,
2. Gia Iko kwenye neutral
3. Washa gari lako
4. Kanyanga Klachi ili uweze kubadili giakwasababu Iko kwenye neutral iwe kwenye gia namba 1
5. Legeza hand breki na kuachilia Klachi pole pole na huku mguu wa kulia ukiwa kwenye accelerator pedal na yenyewe unakanya taratibu gari yako itaanza kutembea
6. Badili gia kwenda namba 2 Kwa kukanyaga Klachi utafanya hivyo huku unaongeza mafuta kwa kunyaga accelerator pedal
7. Ukitaka kusimama utapunguza Kwa kunyaga breki taratibu huku unabadili kwa change down toka labda 4 hadi 2 ndiyo utasimama
Kwenye pikipiki vivyo hivyo lakini Klachi mkono wa kushoto accelerator mkono wa kulia, gia unatumia mguu

Maswali tafadhali
 
Ni kweli mkuu, tunaweka mizengwe mingi sana, lakini hili la udereva linahusu maisha ya watu kwa kiwango kikubwa sana.

Hili la leseni ya udereva tulivumilie
 
Wanasema kwenye pikipiki Kuna kuvuta mafuta nk
 
Naona wauza majeneza wamepata mteja mpya wa haraka sana..
Kwa mara nyingine naona mtu anayeona umauti wake kabla ya kufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…