Sorry for the late reply...umetoa siku amabazo ulitegemea aanze kupata menses (kubleed) ambazo hazisaidii sana. Ungetoa siku alipoanza bleeding kwa mara mwisho ingesaidia zaidi!
Kuna vipimo vingi vya kupima mimba, kutmia damu au kutumia mkojo. Kipimo cha kawaida, kupatikana kirahisi na kinachotumika zaidi ni cha mkojo. Hiki huwa kinapima kiasi cha kichocheo (hormone) kinachoitwa hCG (human chorionic gonadotropin) kwenye mkojo, hormone hii hutolewa baada ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi.
Test za mkojo (UPT) zinazopatika hapa kwetu Tanzania upima hormone hii, na ili kuweza kupatikana kiasi cha kutosha kwenye mkojo ili test iwe positive kwa uhakika inabidi zipite kama wiki 3 tangu tendo lifanyike, au wiki 2 tangu mwanamke akose siku zake. Unaweza ukapima sasa ikasema ni negative ukafurahia halafu baada ya miezi kadhaa dada wa watu anavimba!
Subiri uone kama siku zimechelewa tu (huwa inatokea), zikifika wiki 2 na kuendelea then fanya kipimo cha mkojo cha mimba (UPT), kana ni negative na hatapata siku zake rudia baada ya wiki moja.