Naomba mnijuze hili la vinasaba au DNA

Naomba mnijuze hili la vinasaba au DNA

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2017
Posts
1,503
Reaction score
2,426
Nimefatilia thread nyingi hapa mjengoni na hili linahusu ishu ya DNA kuna baadhi ya nyuzi zili zungumzia upelelezi kwa wahusika wa matukio mbali mbali na kukamatwa kwa njia ya kupima vinasaba wengi wetu tunajua mtu anaweza kamatwa kwa kuhusika na tukio la mahuaji labda kwa kutumia kisu aliua na kisu kikakutwa sehemu husika na alikishika pasipo groves sasa kile kisu kitapimwa kwakua kina alama za vidole kitaonesha na muhusika anaetiliwa mashaka atapimwa ili kuthibitisha na kama ni kweli kahusika itaonesha.

TUJE HAPA PENYEWE
mtoto akizaliwa na baba wa mtoto akiwa na mashaka na uyo mtoto direct ataenda kupima DNA ili kujiridhisha mtoto wa kwake au sio it means DNA inaonesha ishu ipo hapa sasa kwanini mtoto uyo akiua na kuacha alama labda alitumia siraha ya shoka au panga au kisu n.k na wapelelezi wakaingia kati kufatilia akishikwa baba na akapimwa DNA inakataa na akishikwa mtoto akipimwa DNA itathibitisha ndio muhusika wa tukio sasa why DNA iyo iyo mtoto akizaliwa na baba akipima DNA kuthibitisha mtoto ni wake na inakubali lakini kwanin DNA iyo itofautishe kwenye tukio labda la mahuaji wakati watu hao ni damu moja na mbegu moja? Kucha ya baba na mtoto zikipimwa vinasaba vinakubali lakini kucha moja kati ya hao wawili ikikutwa sehemu ya tukio na wote wakachukuliwa kupimwa DNA itamuonesha yule yule aliyehusika na tukio ni swali gumu kulieleza nafikiri nimejitahidi kwa kiasi chake kuliuliza NB watoa povu wapo kila sehem na hata hapa watamwaga tu lakin lengo langu ni kutaka kujua ukiniona mjinga kiasi hicho basi pita kimya kimya ila wenye hekima zao watanijibu bila kukwaza wenzao shukrani wana intelligence.
 
labda kila DNA ina application zake,DNA ya mauaji njia zitumikazo labda ni tofauti na DNA nyingne
ni kama unavyotibu mtu unaweza tumia njia ya operation,vidonge au sindano
 
Kuna chromosome zinazohitakijika kutengeneza genes, binadamu anakuwa na chromosome 23 ambazo anatithi kutoka kwa wazazi wake. Mwili wa binadamu unahitaji 46 chromosomes hivyo 23 zinatoka kwa kila mzazi.

Chromosome ya 23 ni sex chromosome
 
ngoja nikumbukue baioloji ya st. kayumba

katika uzao baba huchangia nusu 23 na mama nusu 23, hivyo upimaji wa d.n.a katika uzazi huangaliwa ufanano wa ule mchango wa baba (e nusu ) kama unaendana na mtoto. hivyo wakikuta unaendana 90%-99% basi huyo atakuaa baba wa mtoto.

katika tukio la mauaji la kumuhushisha baba na mtoto d.n.a haziwezi kuwa sawa, kumbuka mtoto ni mchango wa baba na mama na sio baba tu hivyo kufanya d.n.a kuwa tofauti. nacho fahamu dunia nzima tuna d.n.a tofauti (kila mmoja ana yake)
 
lazima ufahamu kuwa DNA inayo husu mtt kuwa na mahusiano na baba its sex related genes ipo kwenye sex chromomes ambapo saxa genes hiz huwa na taarifa za baba mhusika
matukio ya uhalifu mfano wizi wakutumia silaha unahusisha DNa zilizoko kweny chromosome iitwayo. somatic chromosome (autosomes) body related genes ambazo gene hiz zinabeba taarifa ya mhusika mwenyew
 
Nimefatilia thread nyingi hapa mjengoni na hili linahusu ishu ya DNA kuna baadhi ya nyuzi zili zungumzia upelelezi kwa wahusika wa matukio mbali mbali na kukamatwa kwa njia ya kupima vinasaba wengi wetu tunajua mtu anaweza kamatwa kwa kuhusika na tukio la mahuaji labda kwa kutumia kisu aliua na kisu kikakutwa sehemu husika na alikishika pasipo groves sasa kile kisu kitapimwa kwakua kina alama za vidole kitaonesha na muhusika anaetiliwa mashaka atapimwa ili kuthibitisha na kama ni kweli kahusika itaonesha.

TUJE HAPA PENYEWE
mtoto akizaliwa na baba wa mtoto akiwa na mashaka na uyo mtoto direct ataenda kupima DNA ili kujiridhisha mtoto wa kwake au sio it means DNA inaonesha ishu ipo hapa sasa kwanini mtoto uyo akiua na kuacha alama labda alitumia siraha ya shoka au panga au kisu n.k na wapelelezi wakaingia kati kufatilia akishikwa baba na akapimwa DNA inakataa na akishikwa mtoto akipimwa DNA itathibitisha ndio muhusika wa tukio sasa why DNA iyo iyo mtoto akizaliwa na baba akipima DNA kuthibitisha mtoto ni wake na inakubali lakini kwanin DNA iyo itofautishe kwenye tukio labda la mahuaji wakati watu hao ni damu moja na mbegu moja? Kucha ya baba na mtoto zikipimwa vinasaba vinakubali lakini kucha moja kati ya hao wawili ikikutwa sehemu ya tukio na wote wakachukuliwa kupimwa DNA itamuonesha yule yule aliyehusika na tukio ni swali gumu kulieleza nafikiri nimejitahidi kwa kiasi chake kuliuliza NB watoa povu wapo kila sehem na hata hapa watamwaga tu lakin lengo langu ni kutaka kujua ukiniona mjinga kiasi hicho basi pita kimya kimya ila wenye hekima zao watanijibu bila kukwaza wenzao shukrani wana intelligence.

HABARI,
"mkuu mimi,
Hongera,Hapo swala la uhalifu na kugundulika mtoto na sio baba ni rahisi sana Kwana inaangaliwa tukio lenyewe jinsi lilivyotokea hata kama ndani walikuwa baba na mtoto na akakutwa mtu ameuwawa kwa shoka.Hapo wakiangalia DNA kama ni mtoto itaonekana kwani mtoto anabeba nusu kwa mama na nusu kwa baba itaonyesha huyu muuwaji ni mtoto.Na kama muuwaji ni baba itaonyesha DNA moja iko sawa na ya mtoto hapo ni baba ilanyingine haiko sawa na mtoto hapmojakwamoja itaonekana baba nimuuwaji.

LUMUMBA
 
Kuna chromosome zinazohitakijika kutengeneza genes, binadamu anakuwa na chromosome 23 ambazo anatithi kutoka kwa wazazi wake. Mwili wa binadamu unahitaji 46 chromosomes hivyo 23 zinatoka kwa kila mzazi.

Chromosome ya 23 ni sex chromosome
niliipenda biology ila NECTA ikaipenda zaidi😀😀😀
 
ngoja nikumbukue baioloji ya st. kayumba

katika uzao baba huchangia nusu 23 na mama nusu 23, hivyo upimaji wa d.n.a katika uzazi huangaliwa ufanano wa ule mchango wa baba (e nusu ) kama unaendana na mtoto. hivyo wakikuta unaendana 90%-99% basi huyo atakuaa baba wa mtoto.

katika tukio la mauaji la kumuhushisha baba na mtoto d.n.a haziwezi kuwa sawa, kumbuka mtoto ni mchango wa baba na mama na sio baba tu hivyo kufanya d.n.a kuwa tofauti. nacho fahamu dunia nzima tuna d.n.a tofauti (kila mmoja ana yake)
Hapo umemsaidia ata mimi nimependa jibu lako
 
Kwenye swala la uchunguzi hasa mauaji kesi zake zinachukua muda mrefu sana ktk swala la uchunguzi na ku solve kesi. vinatumika vitu vingi sio DNA pekee kumkamata mtuhumiwa .

Njia wanazotumia kujua au kusolve kesi
nying za mauaji ni
1DNA
2 CCTV cameras
3 Finger print
4Ushahidi wa Mazingira
5Ushahidi wa mawasilino
Lakini kesi nyingi za mauaji zinategemea sana
laboratory kusolve kuanzia DNA mpaka Finger
print ambapo FBI wana
system ya Combined DNA Index System
( CODIS ) ambayo raia wote wa US DNA zao
zinakuwapo so wanakuwa wanafanya matching
na DNA ya kwenye Crime scene pia bado aitoshi
kumfungulia mtu kesi kwani mtu anaweza kuua
na kupadikiza DNA ya mtu mwingine kwenye
Crime scene

NB; nadhani nimekujibu kuhusiana na makosa ya kijinai na mauaji ambapo DNA utumika kuhusu kilichomo ndani ya DNA yenyewe ma Dr wa Jf watakujibu.
 
Kuna chromosome zinazohitakijika kutengeneza genes, binadamu anakuwa na chromosome 23 ambazo anatithi kutoka kwa wazazi wake. Mwili wa binadamu unahitaji 46 chromosomes hivyo 23 zinatoka kwa kila mzazi.

Chromosome ya 23 ni sex chromosome
Duh okay sawa tumekuelewa..ila kama umeishia njiani hivi
 
Back
Top Bottom