Lipijema
JF-Expert Member
- Mar 8, 2015
- 830
- 1,223
Wanajamvi wenzangu naomba msaada wenu mnishauli/ munieleweshe kisheria kuhusu mimi na wapangaji wangu. Hawa wapangaji wapo kwangu sasa ni miaka mitatu tangu nimewapangisha ndani ya nyumba yangu hii, kwa ujumla ninaishi nao kwa amani tu, tatizo lao kubwa kati yao na mimi ni ulipaji wao wa kodi kwa kila mwezi. Mkataba wetu ilikuwa ni kutanguliza kodi ya miezi mitatu mitatu kwa kila muhula, kwa hali ya ubinadamu tu wakati mwingine huwa nawavumilia ili wapatapo wanilipe, sasa basi katika kuvumiliana huku nimejikuta wamelaza kodi ya pango ya miezi saba ndani ya hii miaka mitatu bila ya kunilipa! Nimewataka wahame kwangu kwa vile hii ni dalili ya kutonilipa kwani malimbikizo yamesababisha deni kuwa kubwa, swali ni je, hapa sheria inasemaje kuhusu haki yao na yangu pia? wanayo haki ya kuwapa muda!? Nami kuhusu pesa ninayo wadai je?Msaada wenu wana jukwaa.