Naomba mnijuze,maendeleo ya kiuchumi na mume na mke kuwa waajiriwa vina uhusiano?

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
wanajf naomba mnijuze,eti mume na mke wakiwa wafanyakazi za kuajiriwa ndiyo wanakuwa na maendeleo zaidi kuliko mmojawapo akiwa mfanyakazi mwingine msaidizi wa nyumbani?
 
Wamekudanganya.
Maendeleo ya kiuchumi ya wanandoa ni matokeo ya wanandoa wapambanaji kimaisha wasio wabinafsi.
 
Binadamu wote wenye maendeleo makubwa kiuchumi duniani sio waajiriwa ila kibongobongo mkiwa wote mna ajira mnasaidiana kama mna maelano mazuri mpaka kwenye fedha, kuna baadhi ya wanandoa pamoja na kuwa wote waajiriwa lkn mume hajui mkewe anapokea mshahara kiasi gani wala anazitumiaje, na kuhusu biashara inategemea ni biashara yenye mtaji wa kiasi gani kama ni mkubwa inatosha kuishi maisha mazuri bila mke kuangaika na chochote.
 
kwa tz mmh haiko hivyo, wanawake wengi huwa wabinafsi hukumbatia fedha zao na kuzimaliza kwa vipodozi na mavazi.
 

ndoa nyingi ambazo mume na mke ni waajiriwa, zinakuwa hazina amani na hiyo kufanya wasiwe na mipango ya pamoja ili kujikwamua kiuchumi!
 
Huwa nashindwa kuwaelewa watu ambao wanatafuta kuoa mwanamke aliye ajiriwa au anayetegemea kuajiriwa.
Katika maisha kitu kinachojenga uchumi ni upambanaji. Trust me kuna wadada hata chuo hawajafika lakini ni wapambanaji ile mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…