Ni kweli kwa jinsi ulivyoandika uzi wako ni vigumu kueleweka.
Hatahivyo kama nitakuwa nimejitahidi kukuelwa, ni kwamba
jamaa alifungwa miaka 15 jela kwa kosa la mauaji, alipotoka
alikutana na yule mtu mbaye alituhumiwa kuwa alimuua yaani
yule aliyepaswa kuwa "Marehemu" alikuwa bado yu hai na kwamba
huyo jamaa aliyetokea jela akaamua kumkimbiza na kumkatakata
kwa panga ili amuue akifikiri kuwa adhabu ya kumuua mtu huyo tayari
alishaitumikia hivyo huenda hawezi kuadhibiwa tena.
Kama "senario" ndiyo hiyo jibu lako ni kama ifuatavyo:
Hapa Tanzania kosa la mauaji haliadhibiwi kwa kifungo cha miaka 15, adhabu
ya chini ni kifungo cha Maisha. Vinginevyo huyo jamaa atakuwa alifungwa
kwa kosa la Mauaji ya bila kukusudia " Manslaughter".
Hata kama ni kweli yalifanyika makosa wakati wa upelelezi na ushahidi
mahakamani ukatolewa kuwa "marehemu" alikufa kutokana na kitendo fulani cha
mtuhumiwa, halafu imebainika baadaye kuwa hakufa mtu kwa kitendo hicho, haihalalishi
kumuua sasa baada ya kumaliza kifungo na kumuona"marehemu" yupo hai. Hapo sasa atakuwa
ametenda kosa kubwa la mauaji, kwani vigezo vitakuwa vimekamilika yaani, tendo baya + nia ovu.