Naomba mrejesho kwa alienunua pikipiki kutoka Kupatana

Ukitaka pikipiki njoo nkuzie nnayo PGO SCOOTER miguu 3,cc 150
Nlitoa denmark nmeipiga turubahi
Pikipiki nshachana nazo maana si wengine watu wa kilaji
Nko dar

Ova
 
Duu! Huyo naye alikua bundi yaan unaingiza hela bila kuona chombo
 
Ukitaka pikipiki njoo nkuzie nnayo PGO SCOOTER miguu 3,cc 150
Nlitoa denmark nmeipiga turubahi
Pikipiki nshachana nazo maana si wengine watu wa kilaji
Nko dar

Ova
Chaguo langu n sanya, fekon, au kinglion
Zingne repair ni bei gali mno hasa boxer
 
Ha ha ha mi pia jamaa aliingia mitini baada ya kumwambia niko zenji so nakuja kuchukua mzigo nimpe na cash
Kuna demu yupo instagram anajiita adija_tv kitu kama hicho. Ni mzenji nae anauza tv bei ya kutupa kabisa. Yanii too much sauce mzae!
Lg smart tv 32" unakuta 260k babu, Samsung smart tv 55" unakuta inauzwa 460k binafsi nilimjaribu akaanza kuleta story za kutuma pesa nusu kwanza mzigo unakufikia kokote nikawa nimepatwa na maseke nikambwambia nitaifata mwenyewe nikija huko likizo.
Akapanic akaanza kuntumia mamesej kibao ya watu walionunuaga kwake wakimshukuru kuwa wamepata mizigo yao tayari! Nikahisi ni tapeli tu pia aliejifanya manz ili awapige watu kilaini, hao wafanyabiashara wa zanzibar sikuhizi wengi wapigaji sana wenye uaminifu waliobaki ni wauza ubuyu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…