Wanawake mnakwama wapi kwenye urembo?
Jiulize huko cosmetic wamekushauri utumie Goldie kwa sababu zipi walizotoa wao?
1.Je Goldie ina tibu chunusi?
2.Kwa watu wa ngozi aina gani?
3.Je wewe una ngozi aina gani
4.Sababu za chunusi kwako ni zipi?
Maana kwa swali ulilouliza ni kama vile Goldie ni "one size fits all" yaani inatibu tatizo kwa kila mtu kitu ambacho sio sahihi maana inawezekana ikatibu chunusi kwa mtu wa ngozi Fulani lakini kwa mwingine isitatue tatizo.
Wife alitumia Goldie kwa kushauriwa na rafiki yake, alipoanza kutumia hali ikawa mbaya zaidi ikabidi arudie mafuta aliyoyazoea ndio ngozi ikakaa sawa.
Hasara zake ni kwamba unaingia gharama kununua mafuta ambayo yakikukataa itabidi uyaache uanze kutafuta tena kwa kubahatisha ndio maana bajeti yenu ya kujiremba ipo juu.