Naomba msaada gari lina miss

Naomba msaada gari lina miss

murume

Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
90
Reaction score
80
Wakuu naomba msaada gari lina miss kila asubuhi au kila nikilizima Kwa mdaa mrefu tuseme kama masaa nane ukija kuwasha linakuwa na Miss kubwa tuu hadi linatingishika na kukuwashia taa ya check engine ila likisha changanya Miss inapotea nimebadilisha plug lakini bado kuna fundi kaniambie ni coil je nikweli naombeni msaada make ya gari ni Isuzu wizard
 
mkuu kwa kuwa gari huwa inawasha check engine hembu tafuta fundi akupimie au upo wapi nije nikupimie ndio itakuwa rahisi zaidi kuliko kuanza kufanya olonzi wa kuotea otea waweza ingia garama kubwa ya kununua vitu ambavyo sio vibovu na havisababishi.
 
Diagnosis ni nzuri hapo, japo kama ni coil sio kazi kubwa washa Gari kisha fundi aondoe coil moja moja.

Ajarib kama ina rusha moto kwa kugusisha hapo kwa tundu lake ilipochomolewa wakati ikiwa silent ukiona hairushi moto ndo yenyewe hio.

Mi sio fundi ila nshawai experience hii kitu na haikua plugs ila koil moja haikuwa yafanya kazi.
 
Nenda kwa fundi mwambie afungue sehemu za plug na achomoe coil moja baada ya nyingine huku gari likiwa linawaka sehemu ya plug ambayo utachomoa coil ukaona injini haitikisiki hiyo coil imekufa....Badilisha coil endelea na maisha
 
Hayo yaliyokutokea ndio yamenitokea mimi juzi tu ijumaa nikaenda kufanya diagnosis na kuambiwa system is too lean....Fundi akaenda akachomoa coil moja baada ya moja na kukuta moja imekufa..... nikanunua coil mpya na kufunga na sasa mwendo mdundo......
 
Hivi Haya Majibu ya coil Ni Kwa magari yote tunayotumia na yenye kumiss au Ni Kwa Isuzu wizard peke yao. Mie nina kiji ist sikielewielewi.
 
Nenda kwa fundi mwambie afungue sehemu za plug na achomoe coil moja baada ya nyingine huku gari likiwa linawaka sehemu ya plug ambayo utachomoa coil ukaona injini haitikisiki hiyo coil imekufa....Badilisha coil endelea na maisha
Jaribu hii, isipokuwa sawa fanya engine diagnosis
 
Back
Top Bottom