Naomba msaada kama kuna sheria ya kunisaidia katika hili

ivanmark714

Member
Joined
Jul 13, 2019
Posts
67
Reaction score
110
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 25 na ni wa mwisho kuzaliwa katika familia yenye watoto sita. Wazazi wetu wameshafariki hivyo tumeachiwa baadhi ya mali ambavyo ni nyumba na mashamba tumegawana baadhi ya mali (mashamba) hakuna shida.

Tatizo lipo hapa ninapofanyia kazi mimi ni kwenye nyumba ya familia! Kama ilivyo kawaida mfano ikatokea wanataka tuuze hapa ipo sheria ya mimi nikitaka nigaiwe kasemu ambapo mimi nafanyia kazi kama tulivyogawa sehemu nyengine sababu ni sehemu nyeti ambapo hata ukiwa sehemu ndogo ya kuenea fremu moja inawezesha kuendesha maisha yangu na nikaridhika kwa sehemu hiyo!

NB: poleni kwa uwandishi mbaya
 
Msimamizi wa Mirathi aliyeteuliwa na mahakama kwenye hizo mali ni nani?

Kiufupi mnatakiwa mgawane mali zote mapema iwezekanavyo na ndivyo sheria inavyotaka. Msimamizi wa Mirathi akishateuliwa na mahakama anapewa miezi minne au sita tu ya kugawa mali za marehemu na kufunga jalada la Mirathi mahakamani.

Kuacha Mali za marehemu bila kugawana muda mrefu hupelekea migogoro mikubwa sana siku za usoni mpaka Kwa wajukuu wenu.

Kurudi kwenye swali lako, ni kwamba Mali huuzwa Kwa makubaliano ya warithi, hivyo kama unataka uachiwe sehemu badala ya kuuza mnakubaliana. Nasisitiza iwe mapema na mgawanyo uwe Kwa maandishi upelekwe mahakamani kwenye jalada la mirathi la sivyo italeta shida huko mbeleni.
 
Asante sana mkuu japo hutakuwahi kuwa na msimamizi wala kwenda mahakamani tuligawana kwa makubaliano yetu wenyewe tu...!! Na swala langu umenijibu vyema ni la kimakukubaliano nitajaribu kuliwasilisha asante
 
Mnakubalia na familia kuuza eneo/jengo. Vp kuhusu mnunuzi anaweza kukubali kununua jengo na wewe ukabaki kuwa sehemu ya umiliki?

Jengo linahati? Inawezekana kuuza jengo upande au sehemu na sehemu ikabaki kwa mmiliki wazamani? Kisheria ipo je hii?

Ukijiuliza maswali utagundua kuwa unachokihitaji kitategemea si tu makubaliano ya familia bali na mnunuzi wajengo kukubali kumiliki jengo kwa ushirikiano yaani (co-ownership).

Kwahio swala hili lifikirilie pia kwa upande wa mnunuzi.
 
Asante sana mkuu japo hutakuwahi kuwa na msimamizi wala kwenda mahakamani tuligawana kwa makubaliano yetu wenyewe tu...!! Na swala langu umenijibu vyema ni la kimakukubaliano nitajaribu kuliwasilisha asante
Kama hamkwenda mahakamani mgawanyo wenu ni batili. Na hata mkiuza hiyo nyumba mauziano yatakuwa batili bila barua ya usimamizi wa Mirathi kutoka mahakamani.

Hakunaga shortcut kwenye sheria. Madhara yake mtayakuta mgogoro ukitokea na mkapelekana mahakamani.
 
Asante sana mkuu japo hutakuwahi kuwa na msimamizi wala kwenda mahakamani tuligawana kwa makubaliano yetu wenyewe tu...!! Na swala langu umenijibu vyema ni la kimakukubaliano nitajaribu kuliwasilisha asante
Watu wote waelewe kuwa the fact kwamba baba yako au ndugu yako yeyote wa karibu amefariki na wewe umebaki haimaanishi kwamba automatically mali zake ni zako no, Kuna utaratibu wa kisheria wa kuzihamisha. Marehemu anapofariki Mali zake zinakuwa katika jina lake.

Ndugu wa karibu lazima muombe mahakamani Ili mpate access ya Mali hizo, mahakama itateua msimamizi wa Mirathi ambaye kazi yake ni kusimamia ugawanywaji wa Mali hizo.

Msimamizi wa Mirathi anaweza kuuza hizo mali Kwa ridhaa ya warithi wengine, na mpaka muuzaji ni msimamizi wa Mirathi ndiye atakayekuwa kwenye mkataba wa mauziano.

Kununua Mali ya marehemu kutoka Kwa mtu asiye msimamizi wa Mirathi ni kutapeliwa, hata kama ni mrithi halali Ili mradi hajakabitdhiwa kisheria hana mamlaka ya kuuza Wala kufanya chochote.
 
Asante sana mkuu...!! Nimesoma nikuelewe na nimekuelewa kwa maana hoja yangu ilikuwa ni mimi kutotaka kuuza ila nigaiwe sehem yangu baadala ya kuuza naweza inawezekana kisheria au hiyo ni baada ya kufika mahakamani ndii itajulikana?
 
Uandishi changamoto
 
Umenijibu vizuri sana mkuu ni changamoto kweli kweli apo haswa kwa upande wa mnunuzi lakn kwa jinsi hiyo sehemu ilivyo na impact nitaomba mungu
 
Umenijibu vizuri sana mkuu ni changamoto kweli kweli apo haswa kwa upande wa mnunuzi lakn kwa jinsi hiyo sehemu ilivyo na impact nitaomba mungu
Ingewezekana mkakaa na familia na wewe kama upo vzur mfukoni ukanunua mwenyewe ili kuondoa sintofahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…