Naomba msaada katika hili la kununua nguo

Naomba msaada katika hili la kununua nguo

switmumie

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
7
Reaction score
3
Habari za asubuhi wapendwa.
Yaani nimeamka na mawazo sana nikaona nije huku kutaka msaada wenu yawezekana mm ni mshamba eneo hili.

Juzi nilinunua nguo duka fulan maeneo ya Sinza kulikua na sale hizi nguo za Uturuki kwa sale ya sh laki1. Katika nguo zilizokua kweny sale atleast ile kwangu ndio ilinivutia machoni pamoja na kua zilikuwepo nyingi tu.
Sasa kufika nyumbani nikajaribu tena ile nguo nikiwa kwenye viatu 👠 huku nikitembea tembea kutoka sehem moja kwenda nyingine, nikagundua ile gauni ina kasoro ukitembea kitambaa cha ndani yaani lining inajivuta so gauni inajikunja, wanawake watanielewa.

Basi nikaamua kurudisha pale dukani, kwa vile sikuona nguo niliyoipenda kweny sale nikaona niongeze laki1 nyingine nichukue tu gauni ya kawaida niachane na nguo za sale. Nimechagua nataka kulipa mdada ambae sasa ni mfanyakazi akasema mpigie boss kua unataka kufanya exhange ya style hiyo, kumpigia kanikatalia katakata kwamba haiwezekani sale ni sale na huwez kuchanganya hapo soln ni kubadilisha tu nichukue zilizopo kwa sale, na mm zilizopo sale kwangu sikuona iliyo nzuri. Mwisho wa siku akaniambia kama hamna nguo ya kubadilisha niache then akiiuza atanirudishia hela yangu lakini kufanya top-up ili nichukue nguo ambayo haipo kweny sale hicho kitu hakipo duniani kote, akanitolea hadi mfano wa maduka makubwa kama Woolworths and the like.

Basi nikamshauri mkiwa mnatangaza sale mtoe na hayo masharti ili kina sisi wengine ambao hatuna hizo exposure za maduka makubwa na hatujui kanuni zenu za biashara tujue kuliko hivyo mtu unajikuta unalazimishwa kuchukua nguo usiyoipenda kisa sale, alinijibu shit kwakwel eti hayo hatuwezi kufanya ukifungua biashara yako ndo utafanya hivyo unavyosema😌

Kwa wale wafanyabiashara na wale wazoefu wa haya mambo je ni kweli hiyo exchange niliyotaka sio sahihi au ni yeye tu?. Kwakweli 100K inauma sana maana ile gauni haitauzwa kwa jinsi nilivyojaribu ina shida na mm kupata hela yangu itakua majaliwa aisee🥲🥲

Mnisamehe it’s my first time kupost humu so nimeandika ndefu ili mpate picha ya kile kilichotokea nadhani nimeeleweka. Msinipopoe jamani. Nahitaji mawazo yenu. Asanteni
 
Pole sana usisahau ile sheria ya Buyer be aware. Duniani kote ukiona sale jiule mara 4 kwanini wanaweka sale.
Ukienda shopperz kwa hapa bongo vitu vya sale vyote ni aidha vinakaribia kuisha matumizi au vina kasoro.
Kuna.mashine za kunyolea hazina gia ya kuadjust kiwenbe huwa zinauzwaga kwa sale enzi hizo za game supermarket.

Halafu ukitaka kununua nguo nenda na mtu ijaribu akupe maoni yake usinunue tuu. Hapa bongo vitu vingi ni fake hata hizi juice watu wanazishobikea sijui winniez sijui mack juice sokoni wanaenda kunuana maembe ya bei rahisi yanayokaribia kutupwa ili wapate faida, sijui shake hizi mnakunywa tuu kumbe unajaza.mifunza tumboni
 
Asantee kwakwel nimejifunza kitu. Next time nitakua makini sana
 
Ulifanikiwa kupata pesa yako? Tupe mrejesho
 
Huyo mtu hajui biashara,angejaribu kutumia ubinadamu kwanza,
Pole ,cha kufanya chukua tu hiyo nguo na ukaamgalie namna ya kuiweka sawa ,inaweza ikakufaa kuliko kubishana na mshamba
 
Vipi ulifanikiwa kupata pesaa yakoo.?
Hapana niliamua tu tuchukua nyingine iliyokua kweny sale though sikuipenda kihivyo mana nilijua mwisho wa siku hata ile pesa yangu sidhan kama ningerudishiwa
 
Huyo mtu hajui biashara,angejaribu kutumia ubinadamu kwanza,
Pole ,cha kufanya chukua tu hiyo nguo na ukaamgalie namna ya kuiweka sawa ,inaweza ikakufaa kuliko kubishana na mshamba
Nilibadilisha my dear, thanks kwa ushauri anyway🙏🏽
 
Ulifanikiwa kupata pesa yako? Tupe mrejesho
Hapana nilichukua gauni nyingine ingawa sikuipenda, pesa najua nisingeweza kuipata maana sidhan kama ile gauni kama angeweza kuiza then aje anirudishie hela yangu
 
Uzi wa darisalama wengine hatujui sinza iko wapi
 
Back
Top Bottom