Naomba msaada katika hili, mtoto aliye tumboni ana uzito mkubwa

Naomba msaada katika hili, mtoto aliye tumboni ana uzito mkubwa

Fado

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2016
Posts
237
Reaction score
417
Jana mimi na mke wangu tulienda kumuona Gynacologist, tukaambiwa kuwa mtoto wetu ana uzito ambao alitakiwa awe nao wiki mbele zijazo. Na kwamba kichwa chake kinakuwa pia lakini wamesema hakina maji. Mimba ina week 34 ila mtoto ana uzito wa 2.4gm.
Dr Amesema turudi tena baada ya wiki mbili.

napenda kujua nini husababisha na kama kuna tiba yoyote.
 
Jamani! jamani! mjomba bado hajazaliwa tayari ana kilo 2.4!!
 
Mkuu unamaanisha wewe na mke wako mlienda kumuona Gynecologist au ulimsindikiza mkeo kwenda kumuona huyo mtaalam, kwa maana naamini kama wewe na mkeo mlienda kumuona huyo mtaalam na mkapewa hayo majibu basi ungemuuliza hayo maswali angekupa majibu mubashara BTW ukishapata ushauri tafadhali rudi ukamuone tena mtaalam ukamuulize hayo maswali kama hukumuuliza
 
Gynaecologist anamajibu ya uhakika kuhusiana na maswal yako, jitahid uwasiliane nae umuulize
 
kula sana vyakula vya wanga mama akiwa kwenye miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito ni moja ya sababu.
Hakuna namna, mama ni arekebishe lishe tu, kilo hazipungui, ila awe anaenda kupima tena angalau kila wiki kuona kasi ya uzito kuongezeka kama ni ya kawaida au bado inazidi...
 
Yes kaka, tumeambiwa hivyo so tunaenda tena kila baada ya siku tisa.
 
Mama alikuwa anapenda chapati sana na mayai.
 
2.4 mbona kidogo? mimi sister alikuwa na 2.8 week 34 kajifungua week 36 na 3.8 aliwahishwa kwa sababu za kiafya angesubiria week 40 angekuwa na kilo 5
Aise, sasa ni vyakula au? maana na mimi wangu ameambiwa atembee kila siku kilomita moja ili ajifungue wiki ya 37 na siyo ya 40.
 
Jamani! jamani! mjomba bado hajazaliwa tayari ana kilo 2.4!!
Mkuu usimtishe, 2.4 kg kwa wiki za mwishoni ni uzito mdogo.
Mtoto anahesabiwa ana uzito mkubwa kabla hajazaliwa akianzia 4kg na gramu mia kadhaa.

Huyu kaambiwa uzito mkubwa sababu umri wa mimba na uwiano wa uzito kwa wiki hizo uzito umezidi.

Hapo tatizo kubwa zaidi ni kuwa na maji au damu pungufu. Nafikiri dokta atawasaidia wafanye nini na mama anywe nini.
 
Mdogo wangu alijifungua mtoto 5.1 kwa njia ya kawaida ila alikipata cha moto
 
Back
Top Bottom