Naomba msaada kuelewa kuhusu risiti za ulinzi shirikishi

Naomba msaada kuelewa kuhusu risiti za ulinzi shirikishi

COBOL

Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
98
Reaction score
222
Wakuu habari?

Hapa kwetu kuna watu wamekuwa wakija na kujitambulisha kama Afisa wa Usalama hapo mtaani na wanakusanya mchango wa mwezi, nilimpigia simu mtendaji wetu kama anawafahamu hao vijana akasema ni vijana wao. Wamekua wakija kwa miezi mfano miwili mfululizo na kupotea hata miezi mitatu kisha wanaanza kuja tena.

Nakumbuka tulifanya malipo mara ya mwisho ilikua mwezi wa saba. Siriti za yale malipo walinipatia mkononi, sio kutoka kwenye mashine mfano EFD ni risiti ambayo nilipowauliza kuwa mbona risiti zinatolewa hivi wakasema ni kwamba zinatengenezwa kwanza manispaa halaf wao ndo wanaletewa kufanya makusanyo.

Kila nikifikiria hili swala logic zangu hazikubali kwenye moja, kuna kitu nahisi hakiko sawa. Kuwa kuna uwizi au mchezo akili yangu inahisi unafanyika. Nataka sana kuwa challenge hawa jamaa mpaka akili yangu iridhike. Lakini sijui maswala ya kisheria juu ya hili.

Naombeni ushauri wenu wa kisheria, ni sawa kuwa hivi kwa sheria zetu za Tanzania, au huu ni uwizi?
 
Sio kila kitu kinahitaji sheria. Mambo mengine ni kujitambua tu.
 
Back
Top Bottom