Kaka yangu alifariki Jan 2017. Mei 2017 mirathi ilifunguliwa mahakama ya mwanzo Temeke. August 2017 hundi za pesa za mirathi ziliwasilishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kugawiwa kwa wahusika. Tumefuatilia mahakamani hapo hadi Dec 2017 wakasema faili wamepeleka mahakama ya Wilaya Temeke na kwamba Jan 2018 pesa zitakuwa tayari kwenye akaunti za wahusika. Leo tumefuatilia tunaambiwa faili halijafunguliwa mahakama ya Rufaa na halionekani. Hakika.mjane na watoto wanateseka mnoo!! Maswali yangu kwenu wanataaluma na watendaji katika fani hii,
1. Je ni kawaida kwa mchakato wa malipo kwa hundi zilizokwisha wasilishwa kuchukua muda mrefu kiasi hicho?
2. Je kuna jambo tunakosea au hatujatekeleza ili malipo hayo yafanyike?;Kwa wenye uzoefu.
3. Nani anaweza kutusaidia kwa upande wa mfumo wa Mahakama, wapi tukalalamike au kuomba ufafanuzi??
Ombi langu kwenu wanajukwaa kama kuna yeyote anae weza kutusaidia, tunaomba asaidie kwani kuna watoto wamekwama kwenda shule hadi muda huu, tafadhali tunahitaji msaada!!