[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787] we jamaa mbona unafurahisha. Hizo ziunganishweje na gharama za gari wakati gari umenunua wewe, wao wataijuaje?
Hio hesabu wanayokupa ni tofauti kabisa na gharama za gari lako toka japan.
Ukitaka kupata jumla ya gharama, chukua unayopata kwenye calculator yani kodi, jumlisha CIF (gharama ya gari mpk bandarini), jumlisha gharama za bandarini hizo atakwambia agent wako atakaye clear gari, pia jumlisha pesa ya agent atakaetoa gari bandarini.
[emoji872][emoji872] kumbuka TRA wana formula yao ya kodi inayojenga msingi wake katika makadirio yao ya CIF ya gari husika.
Uki peak gari ambayo wao wanaikadria sokoni bei yake ni kubwa basi kodi pia itakuwa kubwa.
Kadri gari inavokuwa mpya zaidi kwa miaka ndivyo kodi pia inakuwa kubwa, kadri gari inavyokuwa luxury zaidi ndivyo kodi pia huwa kubwa
Kila la heri!