Naomba msaada kujua maandishi haya yana maana gani

Naomba msaada kujua maandishi haya yana maana gani

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
2,351
Reaction score
2,255
Habari wakuu,

Huu uzi nilitaka kuuweka kwenye jukwaa la sayansi na teknolojia lakini nimeona huenda kuna watu ambao hawatembelei kule na wanaweza wakawa na msaada. Kwa kweli ni kama muujiza tu.

Mimi nina kawaida ya kutembea na note book au karatasi na kalamu muda wote ili nikiwa na chochote ninachohitaji kuandika nifanye hivyo. Kuna karatasi ambayo nimekuwa nayo mfukoni kwa takribani wiki tatu na nilikuwa naangalia kama kuna lolote la maana nilihamishie kwenye note book ili niitupe.

Vitu vyote vilivyoandikwa mle nakumbuka vina maaana gani. Nyingi ni namba za simu na maelezo mengine wakati nikiwa na maongezi na watu. Ila nimekutana na haypo maandishi hapo kwenye picha (ya wino mweusi) ambayo sielewi yana maana gani na nani ameandika. Mwenye ujuzi wa kuelewa maana anisaidie. Is it a coded language au ni kitu gani?

2484302_code.jpg
 
Kifupi, kama hujui chanzo chake wala maana yake basi huo ujumbe haukukusudiwa uwe wako? Kwani usipojua maana yake unapungukiwa nini?
Asante but sometimes there are paranormal occurrences that can mean something in life. I am just inquisitive na ndio maana nimekuja kwenye jukwaa kuona kama yeyote anaweza kuelewa chochote nisije nikatupa kwenye dust bin kitu chenye maana. Asante
 
Asante but sometimes there are paranormal occurrences that can mean something in life. I am just inquisitive na ndio maana nimekuja kwenye jukwaa kuona kama yeyote anaweza kuelewa chochote nisije nikatupa kwenye dust bin kitu chenye maana. Asante
Ni karatasi ilikuwa mfukoni kwangu wakati wote ndio maana sielewi
 
Mbona kitu rahisi sana apo umeshindwa nin kuelewa hapo mama kaandaa records ya idadi ya kilo za nyama katika siku saba za week kam ifutavyo

Jt-1 (jumatatu kilo 1)
Al-2(alhamis kilo2)
W-3(Wednesday 3kg)
Nk
Kizinga kinatengenezwa kwa mzee, tulia ule nyama ww
 
Hii wiki hujapitia bar ? Ukute ulikuwa unamuandikia barmaid adondoshe konyagi , Savana na safari ila kwa lugha ya kipombe pombe.
 
WE hicho kikaratasi umekitoa wapi?
Ni cha kwangu mkuu kilikuwa mfukoni kwa muda maana kuna vitu nilikuwa nimeandika na sikuwa na muda wa kuvihamishia kwenye computer au note book
 
Wewe hicho kikaratasi umekitoa wapi.....?
Anyway.....ni namna ya kucalculate siku za period.....kujua siku za hatari.......
Karatasi ni yangu na nimekuwa nikitembea nayo kwa zaidi ya wiki mbili. Kuna vitu vindi nimeandika humo. Ni karatasi ya A4. Sasa huyu aliyeandika calculations zake za period ni nani? Mhh!!!!!!
 
Hii wiki hujapitia bar ? Ukute ulikuwa unamuandikia barmaid adondoshe konyagi , Savana na safari ila kwa lugha ya kipombe pombe.
Nilipita mkuu nikapiga virikuu vichache nikaondoka ila huo si mwandiko wangu!
 
Back
Top Bottom