Naomba msaada kulielewa jambo hili

Sawa umejibu vizuri sana juu ya chimbuko la ibada za jumapili na umuhimu wa siku ya jumamosi kwa wakristo wengine. Tena inaonyesha wewe ni mkristo msomi unayependa kuijua sana imani yako ndio maana unawajua hadi mababa wa kanisa kama uliyemtaja hapo.

Nakurudisha kwenye eneo moja bado ambalo haujaligusa. Siku ya jumapili na siku ya Jumamosi zilitambulikaje hapo mwanzoni? Baada ya binadamu kujiona ameumbwa na yupo duniani, alijuaje kwamba leo ni jumapili, kesho Jumatatu? Je zile siku sita alizofanya kazi ya uumbaji alikuwa ameketi duniani au alikuwa wapi? Kila sayari ina idadi zake za siku na idadi yake ya masaa. Kuna swali la kifilosofia hapa kama umenielewa... Na ukishaweza kulijibu utaweza kwenda hatua ya juu zaidi ya kuisoma na kuielewa imani yako.
 
Asante sana Mkuu kwa somo nimekuelewa barabara
 
Nakujibu kama ifuatavyoo

1.Swali kwamba Mungu alikuwa kasimama wapi usijisumbue kujiuliza maana hutapata jibu ila ni yeye tu wa Kukujibu kwa hivyo Kaza mwendo kumuamini ukifika Mbinguni utamuuliza lakini ntakusaidia kidogo hapo soma Mwanzo 1:2 "Nayo nchi ilikuwa ukiwa ,tena utupu ,na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji Rohoya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji"


2.Kuhusu siku unatakiwa ufahamu kuwa kalenda tunayotumia sasa ni Gregory ambayo siku inaanza saa6 usiku lakin hapo kabla kalenda iliyokuwa inatumika ni ya kiyahudi na ni ya kibiblia pia ambapo siku huanza jioni rejea Mwanzo 1:5 "Mungu akaiita nuru mchana na giza akaliita usiku.Ikawa jioni ikawa asubuh ,siku moja" mpaka hapo umeona siku inaanza jion na kuish pale jion nyingin inapoanza kwa hivo jumamosi inajulikana tangu kitambo saaan maana inatunzwa hadi leo na wayahudi
tukiachana majina ya siku hayo ni majina tu ndio maana kila jamii ina majina tofauti kwa sababu tofauti Hivyo Jumamosi ni ndio sabato hata Quran inathibitisha hilo

3.Kuhusu siku ya kuabudu Biblia ipo wazi kabisaa Kitabu cha Kutoka 20:8 "ikumbuke siku ya Sabato uitakase" ukiambiwa ikumbuke maana yake ni kitu kilichokuwepo Kabla yaani hakijaanza kwa Musa alipopewa Amri 10 na ukirejea katika Uumbaji Mwanzo 2:2 "Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya ,akastarehe siku ya saba .....3. Mungu akaibarikia siku ya saba akaitakasa....." kwa hivo basi neno lipo wazi kabisaa. Pia kuhusu jumapili hizi ni propaganda za kanisa la rumi sababu sio kwamb mitume walikusanyika siku ya jumapili yaan kama ulikuwa hujui ni kwamb karne za mwanz za kanisa la Roman Catholic watu walikuwa wanaabudu Jumamosi?? Fuatilia utagundua hilo na ni kipindi ambapo imani nyingi za kipagani ziliingia kanisani kwa mfano kuna kipindi watu walikuwa wanalipa pesa wanasamehewa dhambi zao yaan unaweza kulipa pesa ukasamehewa hadi dhambi za mwezi ujao [emoji16][emoji16] ilikuwa ni vituko saana na sababu zingin zilizochangia mabadilko haya zinaenda mbaali zaid lakini msingi ndio huo kwamba Kanisa la Roman linahusika kwa 100% na haya madhehebu mengine yanayosali jumapili yalijiengua kutok Roman lakin bad wameendelea kushikilia baadhi ya imani ambazo n za kipagani kama sikukuu za kuzaliwa kwa Kristo hazina mantiki yoyote kwa mkristo halisi kama Huamini soma Luka 1:26 "Mwezi wa 6 malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya jina lake nazareti...." sasa hapo utaona mariam aliipata mimba hio mwezi wa 6 sasa after miezi 9 itakuwa n mwezi wa 3 pengine hata wangeiweka hapo [emoji16] lakin yote na yote hizi sikukuu zilikuwa n za kipagani na ziliingizwa kanisani kwa ajili ya kuongeza waumini....


UKWELI UPO WAZI NI WEWE KUUCHAGUA TU
[emoji117]Mimi nilikuwa muislamu wa kuzaliwa lakin sasa najivunia kuwa mkristo ninae muamini Mungu na mwenye amani tele moyoni sina hofu tena maisha haya ya sasa na sitendi dhambi kwa kuogopa moto au adhabu za kaburini kama ilivokuwa kipind muislamu sasa SITENDI DHAMBI KWA SABABU NAJARIBU KUFANANA NA YEYE ALIENIUMBA YAANI KILA SIKU NAJITAHIDI KUMUAKISI YEYE KATIKA MAISHA YANGU[emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…