Naomba msaada kwa tarehe hizi zipi ni za Mimba?

siku ya 14 tangu siku ya kuanza mens ndio siku ya yai kushuka. Mbegu ya kiume ina uwezo wa kusurvive mpaka siku tatu ikiwa ndani tayari kurutubisha. So kutokea hiyo siku ya 14 hesabu siku tatu kabla mpaka siku tatu baada, nikiwa na maana ya kuanzia siku ya 11 mpaka siku ya 17 ndio kupindi cha kupata ujauzito.

Hiyo tisa, kumi ni kwamba binadamu kutengenezwa ni mipango ya kimbingu, mwenye dunia asiporuhusu hupati ng'o hata ukizingatia vipi huo mzunguko. Akiruhusu fasta tu kitu kinakubali.

Jaribu kugipa gemu kwenye hizo siku then utanipa feedback.
 

wewe kwa mtazamo wangu unacycle mbili ya 21 na 35, lakini kwa kufikiri kwa njia nyingine waweza kuwa na tatizo sasa nakushauri uende hospital ili hii cycle upewe dawa iwe regulated lakini pia ufanyiwe na vipimo vingine kama ultrasonography ili kujiridhisha kama hakuna uvimbe, hii itakusumbua kama ikienda hivi utapata mimba ambazo ujapanga. All the best
 

Kulingana na kalenda yako,mzunguko wako ni wa siku 28,hivyo uwezekano wa kupata mimba ni kuanzia siku ya 12 hadi ya 16. Angalizo: Mume anapaswa kuwa na muda wa kutosha kufanya mbegu ziwe zimekomaa vizuri,asitumie sana pombe au sigara wakati wa kusubiri kukomaa kwa mbegu. Kwa tarehe hzo hapo juu muda wako wa mimba ni kuanzia tarehe 13/4 hadi tarh 17/4. Ukitaka kulenga siku bora,ni ile unapokuwa unapata ute unaovutika uwe mwepesi ama mzito. Wakt huu huwa joto la mwili hubadilika,na huwa unapatwa hamu/ashki kubwa ya kufanya mapenzi. Wakt huo wahi bila kupoteza wakt,haijalish mchana,usiku,ama asubh,ikitokea tu changamka mpe vitu mshua na hutajutia. Ute mzito mtoto wa kike,mwepesi wa kiume. Sababu: mbegu za kike(X) ZINA MKIA MREFU NA ZINA UWEZO MKUBWA WA KUOGELEA Kwenye ute mzito hvy kuziwezesha kulifikia yai mapema na kirahisi na pia wakt wa ute mzito kunakuwa na hali ya tindikali ambayo ni unfavorable kwa (Y) mbegu ume. Mtoto wa kiume ute mwepesi. Timing needed. Kila la heri sis.
 

Mkuu kwa kweli lazima uwe makini maana ukiteleza tu unawezakuwa na mapacha wa nje

Ila utapatiwa maelekezo ya kutosha ili
angalau usijeingia matatizoni.
 
Ninavyofahamu siku za kushika mimba ni kama ifuatavyo,siku ya kumi na moja baada ya hedhi,12,13,14,15,16 na 17.Hizo zote zinauwezekano wa kushika mimba lakini siku ya 14 uwezekano ni mkubwa zaidi.

chukua tano mkuu, uko sawa kbs.
mm nilikutana na mwezi wangu siku ya 15 na sasa hv ni mama kijacho mtarajiwa.
Namshukru sana Mwenyezi Mungu kwa hili tukio.
 
Salam wana jf Dokta.
mwezi huu nijaribu maana mtoto niliye nae ni wa Kike kama hata kuna namna ya kupata wa jinsia nyingine.

Wale tunaoamini katika imani, Jinsi ya kumpata mtoto wa kiume / Kike. Dada lala na ubavu wa kulia wakati wa tendo na ukishamaliza endelea kulala na ubavu huo muda wa nusu saa = Dume na Jike fanya na lala na ubavu wa kushoto muda huo huo. Kama utataka mapacha katika mimba nyingine tuwasiliane kwa PM, ila test kwanza hizo.
Nimetest na nimebahatika Madume 2 niliyoyataka na jike 1 ambayo bahati mbaya alifariki tumboni wiki moja kabla ya mama kujifungua kutokana na homa kali.
 
Mkuu umetisha kwa imani
Lakini nimekukubali sana maana mila
na desturi muhimu lkn pia kuamini kitu
kwakuwa kimekutokea ni vema sana.

Bonge la ujuzi hilo Mkuu
Lete mengine km unayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…