cetterhutter
Senior Member
- Sep 5, 2017
- 167
- 75
Ndugu zangu wanajamvi nimeona niilete maada hii humu ili niliweze kupata msaada kutoka kwenu.
Baba yangu anaumwa kibofu cha mkojo mwezi uliopita hali yake ilikuwa mbaya ikanilazimu nimtumie kiasi cha pesa ili aende hospital ya mkoa Geita.
Kufika kweli kapewa huduma za awali yaani kawekewa mirija ya kukojolea baada ya hapo akaambiwa atoe gharama za upasuaji shilingi 100,000/=pia atoe garama hela ya kununua vifaa kama drip za maji na mengine.
Gharama ikawa kama 86000/=pesa zote zikalipwa na akaambiwa oparesheni itafanyika kesho yake.
Cha ajabu ilipofika kesho yake akaambiwa haiwezekani arudi nyumban kwanza operesheni yake imesogezwa mbele hadi tarehe 18/09/2017 kutokana na wagonjwa kuwa wengi hospitalini hapo.
Kitu cha kushangaza leo tena ameambiwa operesheni yake hadi terehe
02/10/2017 kwa sababu ambazo hazieleweki.
Hapa nipo nawaza sasa nifanyeje kulimaliza hilo tatizo maana nikisema arudi nyumbani gharama ni kubwa.
Kwa wenyeji watakuwa wanaelewa kutoka Kibondo baba yangu anapoishi hadi Geita kuna umbali gani pia ni kiasi gani cha gharama inatumika kwa ajili ya usafiri, malazi pamoja na chakula.
Mimi mwenyewe nipo kibaruani Singida nini nikifanye wadau naomba mawazo yenu.