Naomba Msaada kwa wanaojua taratibu za operesheni

Naomba Msaada kwa wanaojua taratibu za operesheni

cetterhutter

Senior Member
Joined
Sep 5, 2017
Posts
167
Reaction score
75
Ndugu zangu wanajamvi nimeona niilete maada hii humu ili niliweze kupata msaada kutoka kwenu.

Baba yangu anaumwa kibofu cha mkojo mwezi uliopita hali yake ilikuwa mbaya ikanilazimu nimtumie kiasi cha pesa ili aende hospital ya mkoa Geita.

Kufika kweli kapewa huduma za awali yaani kawekewa mirija ya kukojolea baada ya hapo akaambiwa atoe gharama za upasuaji shilingi 100,000/=pia atoe garama hela ya kununua vifaa kama drip za maji na mengine.

Gharama ikawa kama 86000/=pesa zote zikalipwa na akaambiwa oparesheni itafanyika kesho yake.

Cha ajabu ilipofika kesho yake akaambiwa haiwezekani arudi nyumban kwanza operesheni yake imesogezwa mbele hadi tarehe 18/09/2017 kutokana na wagonjwa kuwa wengi hospitalini hapo.

Kitu cha kushangaza leo tena ameambiwa operesheni yake hadi terehe
02/10/2017 kwa sababu ambazo hazieleweki.

Hapa nipo nawaza sasa nifanyeje kulimaliza hilo tatizo maana nikisema arudi nyumbani gharama ni kubwa.

Kwa wenyeji watakuwa wanaelewa kutoka Kibondo baba yangu anapoishi hadi Geita kuna umbali gani pia ni kiasi gani cha gharama inatumika kwa ajili ya usafiri, malazi pamoja na chakula.

Mimi mwenyewe nipo kibaruani Singida nini nikifanye wadau naomba mawazo yenu.
 
Usiombe ukauguliwa wewe, unakuwa kama fuse zimelegea kabisa.
Yaan ww acha mgojwa anapangiwa tarehe ya OPELESHENI kama mahakaman nikiaangalia garama zote zimeshalipwa sjui nikwann au ndio wanataka haad rushwa?
 
Pole kwa tatizo hili jaribu kuongea na wakuu wa idara hiyo katika hospitalini hapo ili uweze kupata huduma kwa muda muafaka.
 
Aides ukiuguza ukawa mpole ,wazweza maliza mwaka nanmzee hajafanyiwa operation. Panda ngapi za juu hapo hapo hospital
 
Yaan ww acha mgojwa anapangiwa tarehe ya OPELESHENI kama mahakaman nikiaangalia garama zote zimeshalipwa sjui nikwann au ndio wanataka haad rushwa?
Mabadiliko ya hizi herufi ni kwa ajili ya kuuguliwa mkuu au hata kabla pole sana
 
Inawezekana presha ya mzee haiko sawa,mshauri aondoe hofu coz oparesheni haiwezi kufanyika bila presha ya mgonjwa kuwa normal
 
Mm nakueleza nione tumtibu mzee wako bila kufanyiwa upasuaji gharama tutarindana mzee cha msingi mlete uku tumnusuru na kisu no:0673303304
 
Back
Top Bottom