Naomba msaada maana ninapata muwasho sana!!

lutamyo

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
641
Reaction score
159
Tafadhari Madokta mliopo JF nisaidieni. Nimekuwa na tatizo la muwasho hasa baridi au maji yanapogusa ngozi yangu hasa nikioga maji ya baridi au nikinyeshewa na mvua. Tatizo hili limedumu kwa takribani miaka 20 ya utu uzima wangu.
Hali niliyonayo inakera sana maana nimalizapo kuoga shutrti nijikune tena kwa zaidi ya dk kumi. Adha niliwahi kwenzda hospitali nilielezwa kuwa ni mzio ila nilazima kwenda Hospitali kubwa. Je ni ugonjwa gani unisumbuao mwenzenu
 
Kama umeshaenda hospitali na hukufanikiwa basi nakushauri upate tiba lishe, hii inaweza kukusaidia sana kwani dada yangu alikuwa anasumbuliwa sana na magonjwa ya ngozi na alihangaika kwa tiba za hospitali hakufanikiwa lkn alipata virutubisho lishe vya kifilipino vikamsaidia na akapona. Ukihitaji ni PM nitakuelekeza mahali pa kuvipata.
 
Pole mkuu, hii kwa kitaalamu inaitwa 'aquagenic articaria', ni aina fulani ya allergy inayotokana na ngozi yako kugusana na maji.

Dawa ya kutibu hakuna lakini wataalamu wa ngozi watakushauri upunguze muda wa kugusana na maji, kama ni kuoga uoge kwa muda mfupi sana, na wakati wote uhakikishe hunyeshewi na mvua.

Ukipatwa na muwasho tumia dawa za jamii ya antihistamines kama cetrizine itakusaidia.
 

Kwa kuongezea tuu mkuu. Unapooga jaribu kutumia medicated soap ambazo hazijachakachuliwa i.e Robert zinasaidia sana kupunguza miwasho ya namna hii
 

Mkuu medicated soaps hazifai
 
Kwa miaka 20 unaumwa tu mkuu, pole sana.

Nakushauri utumie tiba lishe kama alivyoshauri mdau hapo juu, isipokuwa ningekushauri usinunuwe za nje ya nchi, tafuta tibalishe za hapa hapa kwetu.
 
ndugu zang nashukuru mno maana ninateseka mno mkuu gland mal asante, dada ntakupim ila nashukuru mno. mbarikiwe
 
Antihistamine kama cetirizine ni nzuri ila inasababisha usingiza hivyo unaweza kutumia loratadine tabs mkuu pia pole sana kwa yanayokusibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…