AsanteChukua hicho kiasi iliyopo hio ingine waambie mkubaliane wanamalizia lini maana mambo ya kesi yanagharimu sana mda na pesa pia.
hapo ni kuhamasisha kesi yako iende tu mahakamani mkuu, pamoja na kwamba criminal case ni mbaya atafungwa halafu hadi aje atoke ndio ufungue kesi ya madai umdai,..sasa akifungwa miaka 5 ujue utasubiri hadi kifungo kiishe atoke ndio uanze kumdai, utamdai akiwa gerezani kivipi?...pia, wakili au pp anatakiwa kuiomba mahakama mwishoni wakati wa hukumu ikucompensate wewe ulichoibiwa ili iwe kwenye amri ya mahakama kupunguza usumbufu wa aina gani ya njia yako kupata hela yako. kama amri haitotoka, itabidi uje ufungue kesi ya madai akitoka gerezani ukitumia hukumu aliyofungiwa. ningelikuwa mimi ningepambana tumalizane nje ya mahakama.Niliibiwa fedha account ya benk baada ya kufuatilia mtuhumiwa nilimkamata na kumpeleka Polisi ndugu wa mtuhumiwa waliomba tuyamalize pale polisi kabla ya kufika juu zaidi tulikubaliana tarehe ya kunilipa fedha zangu sh laki sita na nusu.
Tarehe husika ilipofika walikuwa wamepata kiasi cha sh laki nne na ilibaki laki mbili na nusu alitakiwa anilipe kiasi hicho tarehe 15/2/2018 cha kushangaza tarehe imefika ananiambia hana pesa, naomba ushauri nifanyeje kisheria?