Lipijema
JF-Expert Member
- Mar 8, 2015
- 830
- 1,223
Wana jf, naamini siku zote ninyi huwa ni msaada mkubwa kwangu, kupitia jukwaa hili nimewasaidia baadhi ya wana jukwaa na ninyi pia nimesha wahi pata msaada wa maelekezo toka kwenu kwa ambayo kwayo yalokuwa yananikabiri. Si unajua tena M/Mungu, alishasema magojwa yote yaweza kuwa na tiba zake isipokuwa kifo na uzee tu!
Nisiwachoshe sana: Mimi nasumbuliwa na jino ambalo linashimo katikati, hili ni jino lile la karibia upande wa mwisho wa jino la chini kulia.
Haka kashimo kanaenda hadi kwenye fizi, taabu inakuja nikikosea nikala chakula kwa kutumia upande huo, basi chembe ya chakula ikitumbukia hapo ndipo huwa nasumbuliwa na maumivu makali sana.
Bila ya kutafunia upande huo hamna shida.Huwa nasikia kwamba kuna utaalam wa kujaza risasi, sijapewa maelezo ya kina juu ya utaalam huu. Naombeni msaada wenu tafadhalini.