Hongera sana ndugu kwa kuwa na wazo
Wengi huanza kama wewe
Mm ni mrombo ila sijawahi kufanya uchunguzi kuhusu kilimo hicho
Pia inategemea na ukanda
Mfano ukanda wa juu ya barabara kuna baridi sana hivyo sikushauri ulime zao hilo
Kama ni chini ya barabara kuna joto
Siyo mbaya kikubwa uwe na chanzo kizuri cha maji na uipende kazi au mradi wako
Kila la kheri
Chunguza bei za nyanya zinavyokua huko mwaka mzima, wapi utauza au utamuuzia nani
Chunguza jinasi ya kuandaa shamba, mbolea, umwagiliaji n.k
Angalia changamoto zake, magonjwa na wadudu ndo wanaweza kukurudisha nyuma zaidi
Mengine wadau wataongezea
Mengine majirani zako wanaolima maeneo hayo watakwambia(hapa uwe makini)
Sasa tumia smartphone yako vizuri humu kuna nyuzi nyingi zinazoongelea nyanya pia search google utapata taarifa nyingi sana